Vazi la BURQA ni Marufuku nchini SENEGAL
Senegal inapanga kupiga marufuku
uvaaji wa vazi la wanawake la Burqa kwa lengo la kuzuia mienendo ya
makundi ya kijihadi,waziri wa maswala ya ndani nchini humo Abdoulaye
Daouda amesema.
Waziri huyo amesema kuwa hatua hiyo haifai kuonekana kama inakiuka uislamu kwa kuwa taifa hilo lina waislamu wengi.
Iwapo mipango hiyo itakuwa sheria,Senegal litakuwa taifa la tano Afrika kupiga marufuku uvaaji wa vazi hilo.
Wiki iliopita ,rais wake Macky Sall,muislamu, alitangaza vita dhidi ya wapiganaji wa kiislamu.
Chad,Gabon na Congo Brazzaville yametangaza marufuku kama hiyo ,huku
Cameroon ikianzisha hatua hiyo mwezi Julai katika jimbo lake la
Kaskazini.
Mataifa yote hayo yalikuwa chini ya ukolini wa
Ufaransa,ambayo ilizua hisia kali mwaka 2011 ilipokuwa nchi ya kwanza
barani Ulaya kupiga marufuku uvaaji wa vazi hilo katika maeneo ya umma .
Mataifa
ya Chad na Cameroon yamelengwa na washambuliaji wa kujitolea muhanga
,wanaohusishwa na wapiganaji wa Boko Haram kutoka Nigeria,ambao
wapiganaji wake mara nyengine huvaa vazi la kujifunika uso ili kuingia
katika maeneo yenye watu wengi.
Post a Comment