Habari za Mahakama ; Wana habari nchini Wafundwa
Rais wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Jaji Mstaafu Thomas Mihayo akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari namna wanavyoweza kuandika habari za Mahakama kwa kuzingatia weledi wa taaluma zao. |
Washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa Habari za Mahakama wakiwa katika picha ya pamoja na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Othman Chande leo jijini Dar es salaam. |
Baadhi ya wanahabari wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa Habari za Mahakama leo jijini Dar es salaam. |
Na Aron Msigwa –MAELEZO
Waandishi wa habari nchini
wametakiwa kuzingatia weledi wa taaluma zao wanapoandika habari za Mahakama ili
kuepuka kuandika habari zinazowatia hatiani watuhumiwa na kushindwa
kutofautisha kati ya mshitakiwa na mtuhumiwa
pamoja na haki zake.
Akifungua mafunzo ya kuwajengea
uwezo waandishi wa Habari za Mahakama leo jijini Dar es Salaam, Jaji Mkuu wa
Tanzania Mhe. Othman Chande amesema
waandishi wa habari wanalojukumu la
kuwapatia wananchi taarifa sahihi kuhusu masuala yanayowahusu na kuepuka
uandishi wa habari zenye kuhukumu.
Amesema kisheria mtuhumiwa huwa hana hatia mpaka
itakapothibitishwa na mahakama kuwa ametenda kosa na kuongeza kuwa kukosekana
kwa weledi katika uandishi wa habari za mahakama huleta mkanganyiko miongoni mwa jamii kuhusu ukweli na kuondoa imani ya watu kwa
mahakama.
Ameongeza kuwa baadhi ya vyombo
vya habari vimekuwa Vikitoa habari
zisizo mpatia mtu fursa na haki ya
kujibu tuhuma huku vingine vikitoa taarifa nusunusu na kushindwa kuwa na mwendelezo
wa habari za mashauri mbalimbali mahakamani.
Mhe.Chande ameeleza kuwa
waandishi wamejikita katika uandishi wa taarifa zenye mvuto kwa jamii na
kusahau nyingine walizo anza nazo jambo
linalosababisha wananchi kuachwa
njia panda bila kupata taarifa za kina kuhusu mwisho wa mambo
yanayoanzishwa.
" Mimi sitaki kuingilia
utendaji wa kazi zenu za kila siku ila nachotaka kusema ni kuweka msisitizo wa
utoaji wa habari za mashauri mbalimbali mnayoanza kuyaripoti kwa mwendelezo ili
msiwachanganye wananchi" Amesisitiza.
Amewataka waandishi wa habari kuandika
habari sahihi na kuepuka upendeleo na maslahi binafsi ili kulinda taaluma na
imani katika jamii juu ya utendaji wa vyombo vya habari.
Mhe. Chande ametoa wito kwa
waandishi wa habari kuepuka uandishi wa habari zilizojaa chuki zinazoweza
kuleta mgawanyiko katika jamii na kusisitiza habari za kuisaidia jamii kukabiliana
na changamoto mbalimbali.
Kuhusu Mahakama amesema
itaendelea kuboresha huduma na miundombinu yake katika maeneo yasiyofikiwa ili
kuendelea kutoa haki kwa wakati pia kushirikiana
na waandishi wa habari wa ndani ili kuimarisha utendaji wao.
Aidha amevipongeza vyombo vya
habari kwa ukomavu viliouonyesha wakati
wa utoaji wa taarifa za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Kwa upande wake Rais wa Baraza la
Habari Tanzania Mhe. Jaji Mstaafu Mhe.Thomas Mihayo akizungumza kwa niaba ya Baraza hilo ametoa
wito kwa waandishi wa habari kuzingatia weledi katika uandishi wa habari za
mahakama ili kuepusha madhara katika jamii.
Amewataka waandishi kujikita
zaidi katika uandishi wa habari zenye uhakika kuliko kuwa na taarifa zenye
mlengo wa kuuza gazeti.
Amesema kuwepo kwa mafunzo hayo
ambayo yameandaliwa na Mahakama ya Tanzania ni ishara nzuri ya uboreshaji wa
taaluma ya habari hasa uongezaji wa ushirikiano katika kutekeleza majukumu ya kimahakama hapa nchini.
Amewataka wanahabari kujifunza na
kufuatilia miongozo na kufuatilia taarifa mbalimbali zinazoweza kuboresha
uandishi wao kwa kupata maneno sahihi ya kimahakama.Amesema Semina hiyo
itawasaidia waandishi wa habari kujenga weledi katika uandishi wa habari za
mahakama.
Ametoa tahadhari kwa waandishi
kuepuka uandishi wa habari zenye uchochezi ili kuepuka kushtakiwa na jamii,
kuepuka lugha za kishabiki na upendeleo.
Naye Meneja wa Maadili wa Baraza
la Habari Tanzania (MCT) Allan Lawa akizungumza kwa niaba ya washiriki wa
mafunzo hayo amewataka kuepuka kuandika habari zinaonyesha upendeleo na kubainisha kuwa kuwa ipo haja kwa vyombo vya
habari kutenga maeneo madawati ya habari hizo
Post a Comment