Header Ads

Rais Dkt JOHN MAGUFULI asaini Kitabu cha Maombolezo Ubalozi wa UFARANSA nchini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha Maombolezo katika Ubalozi wa Ufaransa nchini kufuatia vifo vya Watu zaidi 130 vilivyotokana na mashambulizi ya kigaidi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Malika Berak kufuatia vifo vya Watu zaidi 130 vilivyotokana na mashambulizi ya kigaidi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Ufaransa nchini Malika Berak Tanzania mara baada ya kusaini Kitabu cha Maombolezo na kutoa salamu za pole kwa Rais wa Ufaransa Mheshimiwa Francois Hollande kufuatia vifo vifo vya Watu zaidi 130 vilivyotokana na mashambulizi ya kigaidi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wa pili akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Ufaransa (kushoto) pamoja na Maofisa mbalimbali wa Ubalozi huo mara baada ya kutia saini kitabu cha maombolezo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Malika Berak mara baada ya kusaini kitabu cha Maombolezo Ubalozini hapo.
.............................................

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli amesaini kitabu cha Maombolezo katika Ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es salaam kufuatia vifo vya watu zaidi 130 vilivyotokea November 15, 2015 kutokana na mashambulizi ya ugaidi mjini Paris, Ufaransa.

Pamoja na kutia saini kitabu cha maombolezo, Mheshimiwa Dr. Magufuli ametoa salamu za pole kwa Rais wa Ufaransa Mheshimiwa Francois Hollande na kumuombea uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu.

Dokta Magufuli ambaye amepokelewa na Balozi wa Ufaransa hapa Nchini Bibi Malika Berak amesema Tanzania imeguswa na vifo hivyo na inaungana na Ufaransa katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

Aidha Rais Magufuli amewaombea majeruhi wote wa tukio hilo wapone haraka ili waweze kuungan a na familia zao na kuendelea na shughuli zao za kila siku.

Katika hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli amewasili Mjini Dodoma jioni hii kwa shughuli mbalimbali za kikazi.

No comments

Powered by Blogger.