|
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Sazi Salula,
akizungumza wakati wa Bonanza maalum la kumuaga Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt.
Mohammed Gharib Bilal, liliandaliwa na timu ya timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais
(V.P.O Sports Club) lililofanyika kwenye Uwanja wa Jakaya Kikwete, uliopo
Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam jana Nov 28, 205. Katika Bonanza hilo
lililoshirikisha jumla ya timu Nne za VPO Sports Club, Wizara ya Mambo ya Nje,
Kamati ya Amani waliochanganyika na Mabalozi na Amana Bank waliochanganyika na
Zanzibar Fc, Timu ya VPO Sports Club iliibuka na ushindi kwa kuwafunga Mambo ya
nje kwa jumla ya mikwaju ya penati 5-4 na kutwaa kombe la Bonanza hilo. Picha
na OMR |
|
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Kombe Nahodha wa timu ya VPO
Sports Club, Nehemia Mandia, baada ya kuibuka na ushindi katika Bonanza maalum
la kumuaga Dkt. Bilal, lililofanyika jana Nov 28, 2015 kwenye Uwanja wa Jakaya
Kikwete uliopo Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam. VPO waliibuka kidedea
baada ya kuwafunga timu ya Wizara ya Mambo ya Nje kwa mikwaju ya penati 5-4.
|
|
akamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti cha kushiriki Nahodha
wa timu ya Kamati ya Amani Tanzania, Sheikh Alhad Mussa Salum, katika Bonanza
maalum la kumuaga Dkt. Bilal, lililofanyika jana Nov 28, 2015 kwenye Uwanja wa
Jakaya Kikwete uliopo Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam. VPO waliibuka
kidedea baada ya kuwafunga timu ya Wizara ya Mambo ya Nje kwa mikwaju ya penati
5-4. |
|
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti cha kushiriki Nahodha
wa timu ya Mambo ya Nje, Christopher Mwitula, katika Bonanza maalum la kumuaga
Dkt. Bilal, lililofanyika jana Nov 28, 2015 kwenye Uwanja wa Jakaya Kikwete
uliopo Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam. VPO waliibuka kidedea baada ya
kuwafunga timu ya Wizara ya Mambo ya Nje kwa mikwaju ya penati 5-4. |
|
Nahodha wa timu ya Kamati ya Amani Tanzania, Sheikh
Alhad Mussa Salum, akimiliki mpira mbele ya beko wa VPO Sports Club, Kibiti wakati
wa Bonanza maalum la kumuaga Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, lililofanyika kwenye Uwanja wa Jakaya Kikwete,uliopo Kidongo Chekundu
jijini Dar es Salaam jana Nov 28, 2015.
Katika Mchezo huo VPO walishinda kwa bao 1-0 na kutinga fainali na Timu ya
Mambo ya Nje ambapo pia waliibuka kidedea kwa mikwaju ya penati 5-4 baada ya
mchezo kumalizika bila kufungana. |
Na Muhidin
Sufiani, Dar es Salaam
Timu ya Ofisi ya
Makamu wa Rais, VPO Sports Club, jana Nov 28, 2015 imetwaa kombe la bonanza maalum lililoandaliwa kwa ajili ya
kumuaga rasmi Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kwa kuifunga
kwa mikwaju ya penati 5-4 timu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa katika mchezo wa fainali.
Katika bonanza
hilo lililofanyika kwenye viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Park (JMK Park)
zamani Kidongo Chekundu, timu hiyo iliianza kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya
Kamati ya Amani Tanzania iliyoongozwa na Sheikh Mkuu wa Dar es Salaam, Alhaj
Mussa Salum.
Baada ya mechi
hiyo, Timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais ilicheza mchezo wa fainali dhidi ya
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambayo ilimaliza katika
nafasi ya pili, ilifuzu katika hatua hiyo baada ya kuifunga timu ya Amana Benki
kwa mabao 2-1.
Katika mchezo wa
kutafuta mshindi wa tatu, timu ya Amana Benki iliifunga timu ya Kamati ya Amani
kwa mabao 2-0. Makamu Rais Mstaafu Dk Bilal alishuhudia michezo yote hiyo na
kukabidhi vikombe kwa washindi.
Akizugumza baada
ya michezo hiyo, Dkt. Bilal, aliwashukuru waandaaji wa bonanza hilo kwa kumuaga
rasmi na kusema michezo ina umuhimu mkubwa sana katika maisha ya kila siku ya
binadamu ikiwa ni pamoja na kujenga afya, kuhimarisha na kuanzisha urafiki na
vile vile kuburudisha.
“Nimefurahi sana
kuona jinsi mlivyoonyesha ushindani mkubwa na vipaji vya hali ya juu, sikujua
kama kuna wachezaji wazuri namna hii, nawapa pongezi sana na msiache kuandaa
mabonanza mengine kama haya mara kwa mara, mnatakiwa kufanya kila mara ili
kujenga afya zenu na kuanzisha na kudumisha urafiki na amani” alisema Dkt
Bilal.
Aidha Dkt. Bilal alitoa wito kwa wanamichezo nchini
kutumia uwekezaji huo mkubwa kutoka kwa Rais Mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete
kuendeleza vipaji. “Hapa kuna viwanja vya mpira wa miguu, mpira wa
kikapu, netiboli, mpira wa mikono, mpira wa wavu, tumieni fursa hii kwa
ajili ya kuendeleza vipaji na kuiwezesha nchi kufanya vyema katika michuano ya
Kimataifa,” alisema.
Post a Comment