Header Ads

UNDP yakabidhi Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia nchi

IMG_9773
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Awa Dabo akikata utepe kuzindua Kisima cha maji safi na salama katika kijiji cha Machali A wilayani Chamwino mkoa wa Dodoma mwishoni mwa juma lililopita.

Na Modewjiblog team, Chamwino

KIJIJI cha Manchali kilichopo wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, kimekabidhiwa mradi wa dola za Marekani 150,000 wenye lengo la kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Mradi huo ulikabidhiwa kijiji hicho na Mratibu wa mashirika ya Umoja wa mataifa nchini na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Bw. Alvaro Rodriguez.

Mradi huo umelenga kusaidia jamii inayoishi katika kijiji hicho kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Mradi huo wa nishati ya jua umelenga kutatrua tatizo la nishati na kufanya matumizi bora ya ardhi na teknolojia ya maji.Mradi huo unasaidia familia 600.

Kwa uzoefu wa Tanzania na maeneo mengine duniani, familia maskini ndizo zinazopigika vibaya na mabadiliko hayo na ndio haizna uwezo wa kukabiliana nayo.

Kwa mradi huo wananchi wa Manchali wanatarajia kukabiliana vilivyo na mabadiliko ya Tabia nchi.

Akizungumza katika kijiji hicho cha Manchali, Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Bi. Awa Dabo alisema kwamba ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi uwezeshaji wananchi kiuchumi ni muhimu sana ili kufanya familia kustawi.

IMG_9772
Kisima kilichozinduliwa na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Awa Dabo.

“Athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa watu maskini ni kubwa na ndio wanaoathirika zaidi” alisema Mkurugenzi Mkazi UNDP Bi. Dabo.

Aidha alisema kwamba anaishukuru serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuhangaikia suluhu ya watu kukubali kuwapo kwa mabadiliko ya tabia nchi na kufanya juhudi ya kukabili hali hiyo.

“Hii imo katika malengo ya maendeleo endelevu kwani malengo manne kati ya 17 yanahusiana na mabadiliko ya tabia nchi na kuhifadhi mazingira.kwa kutumia fedha kutoka kwa wadau wa maendeleo, UNDP imefanikiwa kusaidia wananchi wa kijiji cha Manchali kufanyia kazi maeneo kadha muhimu ili kufanya uragibishi kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, kuongeza kasi ya upoandaji wa miti na matumizi ya nishati jadidifu.” alisema.

Bi Dabo amesema kwamba mradi huo wa Manchali umekamilika ni mmoja wa mradi yenye mafanikio inayosimamiwa na UNDP.

Aliwapongeza wananchi wa Manchali kwa ushiriki wao na kuufanya mradi huo kuwa wakwao hali iliyosababisha kuwepo na matunda yenye tija katika kijiji hicho.

“Sisi UNDP kutokana na mafanikio haya tunaangalia maeneo mengine ya kufanya mradi kama huu” alisema Bi Dabo.

UZINDUZI-MRADI
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja waMataifa la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akizindua mradi wa kupunguza na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia nishati jadidifu ya jua (Mitigating Climate change in vulnerable communities of Dodoma region, Machali village, Chamwino District), kijijini humo.

Naye Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Bw. Alvaro Rodriguez alisisitiza ushiriki wa wananchi katika kufaniukisha miradi na kusema kwamba mradi huo umefanikiwa kutoka na ushiriki wa wananchi na hasa kitendo chao cha kuufanya mradi huo kuwa mali yao.

Aliongeza kwamba kitendo cha kufanya mradi wao na kuwa viongozi wa maendeleo yao wao wenyewe kumefanya mradi uwe na tija kubwa kwao.

“Mradi huu umeleta maendeleo makubwa kwa wananchi wa hapa kutokana na wao kuanza kutumia nishati jadidifu, watoto wanakwenda shule na maeneo yameanza kurejewa na misitu.”

Mratibu huyo aliongeza kwamba mabadiliko ya tabia nchi ni ya kweli na wala si ya kuyafanyia mzaha, mashirika ya umoja wa mataifa na Umoja wenyewe wanatazama sana athari zake mbaya.

Alisema kijiji cha Manchali kimefanikiwa katika kuanza kukabili mabadiliko ya tabianchi kwa kubadili mambo yanayowazunguka na kurejesha uoto wa asili na kuacha kuharibu mazingira huku shughuli za maendeleo zikichukua sura mpya yenye kujali mabadiliko ya tabia nchi.

IMG_9802
Bango la mradi uliozinduliwa na Bw. Alvaro Rodriguez.

IMG_9786
Kutoka kushoto ni Mwakilishi Msaidizi wa Shirika la UNFPA, Dk. Hashina Begum, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Awa Dabo, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja waMataifa la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na viongozi wa kijiji wakiwakilisha wananchi ambao watanufaika na mradi huo.

IMG_9842
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Awa Dabo, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja waMataifa la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na Mwakilishi Msaidizi wa Shirika la UNFPA, Dk. Hashina Begum katika picha ya pamoja.

No comments

Powered by Blogger.