KENYA, UGANDA zaimarisha hali ya Usalama
Uganda na Kenya zimeimarisha usalama
kufuatia mashambulio yaliyotekelezwa mjini Paris mwishoni mwa wiki,
kuzuia mashambulio kutoka kwa wapiganaji wa Kiislamu.
Msemaji wa
polisi nchini Uganda amesema polisi na wanajeshi wameimarisha doria
kuzuia mashambulio, hasa kutoka kwa wapiganaji wa Kiislamu wa al-Shabaab
kutoka Somalia.
“Kama tahadhari, tumeimarisha usalama na kiwango
chetu cha tahadhari na pia tukaongeza maafisa wa usalama. Kuna maafisa
wa usalama saa 24 katika maeneo yenye watu wengi,” Bw Enanga alinukuliwa
na gazeti la serikali la New Vision.
Nchini Kenya, usalama pia umeimarishwa mpakani na katika miji mikuu, gazeti la kibinafsi la Standard limeripoti.
Polisi
zaidi walitumwa Jumapili kulinda makanisa na maduka makubwa pamoja na
maeneo yenye kukusanyika watu wengi, gazeti hilo linasema.
Mwandishi
wa BBC David Wafula amewapata maafisa wa Vijana wa Huduma kwa Taifa
(NYS) wakitumiwa kukagua watu wanaoingia katika maduka ya jumla.
"Tunapondelea kuimarisha doria, tunawataka wananchi pia wawe macho,” mkuu wa polisi Joseph Boinnet amesema.
Al-Shabab waliua watu 150
waliposhambulia Chuo Kikuu cha Garissa mwezi Aprili mwaka huu na
watu 67 katika shambulio jumba la kibiashara la Westgate jijini Nairobi mwaka 2013.
Nchini Uganda,
mashambulio mawili ya al-Shabab mwaka 2010 yaliua watu 70.
Post a Comment