Hatma ya Kuagwa ama Kutoagwa Jijini MWANZA mwili wa ALPHONCE MAWAZO ni Kesho
Na George Binagi
Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza leo imeahirisha
kesi ya madai ya kuomba ridhaa ya kufanya ibada ya Mazishi ya aliekuwa
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Mkoani Geita Marehemu
Alphonce Mawazo iliyowasilishwa na Mchungaji Charles Lugiko ambae ni baba mlezi
wa marehemu Mawazo.
Katika kesi
hiyo, mlalamikaji anaiomba mahakama kuondoa zuio la jeshi la polisi Mkoani
Mwanza la kutoruhusu shughuli ya kuuaga mwili wa marehemu Mawazo kufanyika
Jijini Mwanza, kabla ya kwenda kuzikwa Mkoani Geita.
John Mallya
ambae ni miongoni mwa Mawakili watatu wa Chadema ambao wanaitetea kesi hiyo,
amebainisha kuwa Mahakama imeahirisha kesi hiyo hadi kesho majira ya saa saba
mchana, ambapo Jaji wa Mahakama hiyo Mhe.Lameck Mlacha anatarajiwa kutoa
maamuzi yake baada ya leo kusikiliza utetezi wa pande zote mbili zinazohusika.
Kaimu Katibu
Mkuu wa Chadema bara Salum Mwalimu, amewasihi wanafamilia pamoja na wafuasi wa
chama hicho kuendelea kuwa watulivu, wakati maamuzi ya mahakama hiyo yakisubiriwa
ambapo ameeleza kuridhika na mwenendo wa kesi hiyo.
Nje ya
Mahakama, ulinzi ulikuwa umeimarishwa zaidi ambapo kulikuwa na polisi wa
kutuliza ghasia waliokuwa na bunduki za risasi za moto, mabomu ya machozi
pamoja na mbwa ambapo baada ya kesi hiyo kuahirishwa, umati mkubwa wa wananchi
uliokuwa umetanda mita chache kutoka Mahakamani hapo ulianza kuimba nyimbo za
maombolezo na kuwasindikiza viongozi mbalimbali wa chedema hadi katika hoteli
waliyofikia.
John Mallya ambae ni mmoja wa Mawakili wa Chadema akizungumza baada ya kesi kuahirishwa.
Katibu Mkuu Msaidizi Chadema bara, Salum Mwalimu akizungumza baada ya kesi kuahirishwa.
Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe akizungumza baada ya kesi kuahirishwa.
Viongozi na makada wa Chadema wakiwa mahakamani.
Viongozi na makada wa Chadema wakiwa mahakamani.
Mawakili na Viongozi/Makada wa Chadema wakitoka Mahakamani.
Wananchi na wafuasi wa Chadema wakitoka Mahakamani huku wakiimba nyimbo za maombolezo.
Wananchi na wafuasi wa Chadema wakitoka Mahakamani huku wakiimba nyimbo za maombolezo.
Wananchi hawa waliwasindikiza viongozi wa chadema hadi hotelini.
Post a Comment