MSAADA...MSAADA wa Matibabu kwa Dada JOYCE unahitajika
Napenda
kutumia fursa hii kukushirikisha habari ya kusikitisha kuhusu dada
Joyce Mwambepo (pichani akiwa na mwanaye wa miaka 4, na miguu yake
iliyopooza) mkaazi wa Sinde jijini Mbeya. Dada huyu mwenye umri wa miaka
27 anaishi na bibi yake mwenye umri wa miaka 80 pamoja na huyo mwanaye.
Kwa
bahati mbaya mwezi April mwaka jana wa 2014 dada huyu alipata ajali ya
kugongwa na gari ambayo haikusimama kumsaidia. Ila kwa msaada wa
wasamaria wema alipelekwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mbeya ambako
inasemekana alikaa kwa miezi mitatu bila kupata matibabu, kwa kukosekana
nyenzo za kumfanyia uchunguzi.
Katika
uchunguzi wa awali ilibainika kuwa Joyce amevunjika miguu yote miwili,
hivyo akahamishiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili ambako pia baada
ya kukaa kwa miezi kadhaa alirejeshwa tena Mbeya baada ya kukosa
shilingi 550,000/- za vipimo na matibabu.
Hadi
nakutana naye dada huyu alikuwa amelala nyumbani kwa bibi yake (pichani
kushoto) ambaye ni mlezi wake tangu akiwa na miaka minne baada ya
wazazi wake wote wawili kufariki dunia.
Hawezi kukaa wala kusimama na anajisaidia hapo hapo kitandani kwa msaada wa mwanaye huyp na bibi yake. Inasikitisha.
Hivyo
nimejitahidi kufuatialia ili kujua mahitaji halisi lakini ili kumsaidia
Joyce inatakiwa aanze mchakato (process) upya za matibabu kuanzia hapa
Mbeya referral Hospital hadi Muhimbili jijini Dar es salaam.
Gharama za matibabu ni kama ifuatavyo:
1. shilingi 300,000/- za kupima CT-SCAN
2. Shilingi 250,000/- za MRI
3. Usafiri wa kutoka Mbeya-Dar kwa gari maalum la kukodi 700,000/-
4. Gharama za msaidizi ambaye ni rafiki yake 300,000/-
5. Chakula 450,000/- (Endapo watakaa hospitali mwezi mzima)
6. Gharama za matibabu (CT-SCAN&MRI ni vipimo tu) 500,000/-
7. Na mahitaji mengineyo wakiendelea kupata tiba 500,000/-
Hivyo
kwa kuanzia kiasi cha shilingi 3,000,000/- (milioni tatu) kinahitajika
kumpunguzia mateso dada yetu huyu. Asante sana kwa moyo wako wa kujitoa
na Mungu atakubariki.
Deo Kakuru Msimu
Msamaria mwema
+255769 512 420
Wakati huo huo kwa niaba ya Michuzi Media Group, Ankal amejitolea kusaidia uratibu wa kufanikisha matibabu ya dada Joyce. Hivyo unaweza kuwasiliana naye kwa email issamichuzi@gmail.com ama whatsapp namba +255 754 271266 kwa jina la Ankal.
--------------------------------------
UPDATES:
Wasamaria
wema kadhaa wamejitokeza kumsaidia dada Joyce. Hatuna uhakika kwamba
wote wanapenda majina yao yawekwe hadharani, Ila tunapenda hadi sasa
kukiri upokeaji wa Tshs:
1. 505,000/-
2. 50,000/-
3.100,270/-
4. 10,000/-
5. 100,000/-
6. 500,000/- (ahadi ya uhakika)
7. 500,000/- (Michuzi Media Group)
7. 800,000/- (Kulipia gharama za vipimo vya CT Scan Regency Hospital mgonjwa atapofikishwa Dar es salaam).
Hivyo ndiyo kusema jumla ya Tshs. 2,565,270/- tayari zimekusanywa kumsaidia dada yetu huyu anayeteseka. Kwa niaba ya mgonjwa tunashukuru sana kwa msaada huo, hana cha kuwalipa zaidi ya kuwaombea kwa Mola mzidishiwe pale mlipopungukiwa.
Pamoja
na yote hayo, kiasi cha Tshs. 3,000,000/- za ziada zinahitajika kwa
ajili ya kuhitimisha zoezi lote hili. Hiyo ikiwa ni gharama za usafiri,
malazi ya mgongwa na wasaidizi wawili kwa mwezi mmoja (atapopelekwa Dar
es salaam kwa vipimo na matibabu) ili kumsaidia. Hivyo michango zaidi
inahitajika kumuokoa dada Joyce. KUTOA NI MOYO.
Aidha,
kwa kiasi kilichopatikan, mipango imeshafanywa kumpeleka dada Joyce
katika hospitali ya rufaa ya Mbeya kwa uchunguzi mpya wa awali. Baada ya
hapo tutawafahamisha nini kinachotakiwa kuendelea.
Deo Kakuru Msimu
Msamaria mwema
+255769 512 420
Wakati huo huo kwa niaba ya Michuzi Media Group, Ankal amejitolea sio tu kuchangia bali pia kusaidia uratibu wa kufanikisha matibabu ya dada Joyce. Hivyo unaweza kuwasiliana naye kwa email issamichuzi@gmail.com ama whatsapp namba +255 754 271266 kwa jina la Ankal.
Post a Comment