Msaada Wahitajika Kwa Mapacha Walioungana
Hawa
watoto Zahra na Zarina wamezaliwa pacha walioungana tarehe 16/11/15
mama yao Bi Tausi Hageze akiwa njiani kwenye boda boda akitokea kijiji
cha Nyarurema Tarafa ya Rulenge Wilaya ya Ngara akielekea hopitali ya
misheni Rulenge.
Alipopata uchungu wa kuzidi alimuomba bodaboda asimame akaweza kujifungua kwa shida mbele ya mumewe anaeitwa Hamdani hapo njiani.
Alipopata uchungu wa kuzidi alimuomba bodaboda asimame akaweza kujifungua kwa shida mbele ya mumewe anaeitwa Hamdani hapo njiani.
Baada
ya hapo wakapelekwa hospitali ya misheni Rulenge. Mama na watoto wako
salama, kama unavyo ona katika picha wameungana kiunoni. Msamaria
amekutana na changamoto hii hapo hospitali na kuamua kuwasaidia
kuchangisha iliwapelekwe Mwanza Bugando Hospital walipo hivi sasa.
Inaelezwa na ma daktari hapo wameshauri watoto wapelekwe India kwa upasuji na matibabu zaidi.
Msamaria anaewasaidia Bi Sabra Said Salum wa namba ya simu +255767220099 anaomba
yoyote atakae guswa na kadhia hii afikishe mchango kwake ili aweze
kuwafanyia safari hii muhimu kuokoa maisha ya mapacha hawa.
Baba
Hamdani Sibhoro na mama Tausi Hageze wote ni wakulima wa jembe la mkono
hawana uwezo hata wa kufika Dar.
Bi Sabra kachangisha na kuweza kuwafikisha Bugando, kuwalipia mahitaji ya hapo.
Bi Sabra kachangisha na kuweza kuwafikisha Bugando, kuwalipia mahitaji ya hapo.
Mungu awabariki
Post a Comment