Sherehe za Diwali zachafua Hali ya Hewa INDIA
Viwango vya uchafuzi wa hewa huko
mjini Delhi nchini India vimeongezeka pakubwa hasa wakati wa usiku wa
sherehe za jamii ya Wahindi, sherehe za Diwali, vikifikia mara 40 zaidi
ya viwango vinavyopendekezwa na wataalam wa kimataifa, hayo ni kwa
mujibu wa shirika la afya duniani WHO.
Hii ni kwa sababu ya kiwango kikubwa cha fataki ambazo zimekuwa kikifyatuliwa wakati wa shererhe hizo.
Kwa mfano Jumatano usiku vilifikia kiwango cha chembe chembe PM10 katika eneo lililopimwa ambacho ni hatari sana.
Kabla ya sherehe kuanza serikali ilikuwa imetoa wito watu wasitumie fataki katika sherehe hizo.
Gazeti la The Times of India hapo Jumatano lilikuwa limeripoti kuwa hali ya hewa imekuwa mbaya sana.
Viwango
vya kemikali ya sulphur dioxide, ambayo inajulikana kuchochea pumu na
maradhi mengine ya kupumua nayo pia ilikuwa ilikuwa juu katika maeneo
mengi.
Uchunguzi wa WHO wa mwaka 2014 uligundua kuwa kati ya miji
20 iliyo na viwango vikubwa vya uchafuzi wa hali ya hewa duniani, 13
iko katika taifa la India, huku mji wa Delhi ukitajwa kushikilia nafasi
ya kwanza ya miji iliyona uchafuzi zaidi wa hewa duniani.
Kuvuta hewa iliyo chafu imeorodheshwa kama mojawapo ya mambo
yanayosababisha vifo vya mapema huko India, Takwimu zikionesha kuwa
zaidiya watu 620,000 hufa kila mwaka kutokana na maradhi yanayochochewa
na kupumua hewa iliyochafuliwa, WHO imesema.
Mambo mengine
yanayoongezea uchafuzi wa hewa ni kuchomwa kwa maelfu ya tani za taka za
mashambani, viwandani na hata taka za majumbani.
Post a Comment