Watakaokwamisha Juhudi za Dkt JOHN MAGUFULI Sekta ya Elimu Kukiona
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. George Mcheche Masaju akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wahitimu wa kidato cha nne wa shule za Fedha. |
Picha/Habari na Hassan Silayo
Wananchi wameshauriwa
kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano za kuendeleza sekta
ya elimu kwa maslahi na maendeleo ya watoto na nchi kwa ujumla.
Hayo yamesemwa
na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. George Mcheche Masaju wakati wa Mahafali ya
Shule za Sekondari za Wavulana na Wasichana za Feza leo Jijini Dar es Salaam.
Bw. Masaju
alisema kuwa anatambua Serikali inayoongozwa na Rais John Pombe Joseph Magufuli
imeamua na kuelekeza kwamba kuanzia Januari 2016 elimu itolewe bure kuanzia
ngazi ya awali (Kindergarten) hadi kidato cha nne ikiwa ni njia ya
kuwafanya watoto wa shule za msingi au watoto waliofalu na kupata nafasi ya
kusoma elimu ya sekondari kutokusoma.
Masaju alisema
kuwa Asiwepo mtu atakayesababisha mtoto kukosa haki yake ya kupata elimu kwa
sababu yoyote ile ikiwemo kuwaozesha watoto, kuwapa ujauzito, kuwaficha
majumbani, kuwaachisha masomo, kuwatorosha shule, utoro kwani kama nilivyoeleza
awali kufanya hivyo ni kutenda kosa la jinai chini Sheria ya Elimu na Kanuni
zake hivyo serikali itachukua hatua dhidi yake.
“Kama tunavyofahamu
Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Pombe Joseph Magufuli imeamua
na kuelekeza kwamba kuanzia Januari 2016 elimu itolewe bure kuanzia ngazi ya
awali (Kindergarten) hadi kidato cha nne, hivyo asiwepo mtu atakayekwamisha juhudi hizi
kwa njia yoyote ile kwani ni kuwanyima watoto haki yao ya kikatiba kwani Serikali
haitasita kuchukua hatua stahiki za kisheria dhidi ya watu wanaojihusisha na
vitendo hivyo” Alisema Masaju.
Pia Bw. Masaju alizitaka shule na taasisi za elimu kutoa fursa sawa
kwa wanafunzi wote kutumia haki ya uhuru wa kuabudu kulingana na imani za dini
zao kwa kupanga mitihani au vipindi kwa muda au siku za kuabudu kwani ni kukiuka
masharti ya Ibara ya 19 inayotoa haki ya uhuru wa kuabudu.
Aidha Masaju
alizipongeza sekta binafsi za elimu kwa kutoa mchango mkubwa katika utoaji wa
elimu hapa nchini kwa kuongeza wigo wa utoaji wa elimu ya msingi na elimu ya
sekondari; kuongeza vyanzo vya kodi na hivyo kukuza uchumi na huduma za kijamii
kutokana na kodi inayolipwa na shule zinazotoa huduma ya elimu; kutunza na
kuendeleza utamaduni wa Kitanzania kwa kuwezesha watoto kusoma hapa Tanzania
badala ya kupelekwa kusoma nje ya nchi; na kuongeza ajira kwa walimu na watu wa
kada mbalimbali wanaoajiriwa na shule binafsi.
Post a Comment