STARTIMES yateta na Mawakala Wake
Baadhi ya mawakala wa StarTimes Tanzania wakisoma vipeperushi wakati wa hafla iliyoandaliwa kwa madhumuni ya kutoa ufahamu zaidi wa sera na huduma mpya za kampuni hiyo. Anayeonekana mbele akifafanua jambo na kusikilizwa kwa makini ni Meneja wa Operesheni, Bw. Gaspa Ngowi. StarTimes imejiwekea utaratibu wa kukutana na mawakala wake wakubwa na wadogo mara kwa mara ili kujadili mustakabali wa huduma na bidhaa wanazozitoa kwa wateja wao.
Meneja Masoko kitengo cha chaneli na vipindi vya StarTimes Tanzania, Bi. Paulina Kimweri (mbele) akifafanua jambo kwa mawakala waliohudhuria hafla iliyoandaliwa kwa madhumuni ya kutoa ufahamu zaidi wa sera na huduma mpya za kampuni hiyo. StarTimes imejiwekea utaratibu wa kukutana na mawakala wake wakubwa na wadogo mara kwa mara ili kujadili mustakabali wa huduma na bidhaa wanazozitoa kwa wateja wao.
Meneja Mauzo wa StarTimes Tanzania, Bw. David Kisaka (mbele) akifafanua jambo kwa mawakala waliohudhuria hafla iliyoandaliwa kwa madhumuni ya kutoa ufahamu zaidi wa sera na huduma mpya za kampuni hiyo. StarTimes imejiwekea utaratibu wa kukutana na mawakala wake wakubwa na wadogo mara kwa mara ili kujadili mustakabali wa huduma na bidhaa wanazozitoa kwa wateja wao.
Meneja Mauzo wa StarTimes Tanzania, Bw. David Kisaka (mbele) akifafanua jambo kwa mawakala waliohudhuria hafla iliyoandaliwa kwa madhumuni ya kutoa ufahamu zaidi wa sera na huduma mpya za kampuni hiyo. StarTimes imejiwekea utaratibu wa kukutana na mawakala wake wakubwa na wadogo mara kwa mara ili kujadili mustakabali wa huduma na bidhaa wanazozitoa kwa wateja wao.
Na Mwandishi Wetu
Kampuni ya StarTimes Tanzania mwishoni wa wiki hii waliandaa hafla fupi kwa mawakala wake wote nchini ikiwa ni utaratibu iliyojiwekea kwa lengo la kuwakutanisha kujadili juu ya huduma na bidhaa wanazozitoa kwa wateja wao.
Kampuni hiyo imesema kuwa tukio kama hilo huwa linafanyika mara kwa mara pale wnapokuwa na sera pamoja na huduma na bidhaa mpya wanazozitarajia kuzitambulisha kwa wateja.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo Meneja Mauzo wa StarTimes Tanzania, Bw. David Kisaka amesema kuwa kampuni yao kila kukicha inakuwa na hivyo inahitaji mawakala wengi zaidi ili kuweza kumfikia kila mtanzania.
“StarTimes tunayo furaha kubwa kwa kuendelea kujiongezea wateja kila kukicha ambao kwa sasa wanafika takribani milioni moja na kuzidi. Hivyo basi kutokana na idadi hiyo kubwa ni dhahiri kabisa kuwa kampuni haiwezi kuwafikia kwa jitihada zake. Mawakala wetu tunapenda kufahamu kuwa nyinyi mna nafasi kubwa sana kwetu kwani nyie ndio mnakutana na wateja moja kwa moja.” Alisema Bw. Kisaka
Aliongezea kuwa, “Na katika kuhakikisha mnawafikia vema na kuwapatia taarifa sahihi na zinazokwenda na wakati, mkutano kama huu ni muhimu. Umuhimu wake unakuja pale ambapo tunakuwa na sera pamoja na huduma na bidhaa mpya au ofa tunazotaka kuzitambulisha kwa mara ya kwanza sokoni. Tunaamini kuwa bila nyinyi kuzielewa basi itakuwa ni vigumu kwa wateja pia. Hivyo basi hafla hii fupi italenga katika Nyanja hizo pamoja na kusikiliza ushauri wenu.”
Akijibu swali la wakala Bijampora ambaye duka lake lipo Magomeni Mwembechai, aliyeuliza kuhusu kusuasua kwa huduma kwa wateja, Bw. Kisaka amefafanua kuwa StarTimes kwa sasa wamejipanga kwa hilo na tayari kitengo hicho muhimu kimekwishatanuliwa kwa kuajiri wafanyakazi wengi zaidi.
“Kitengo chetu cha huduma kwa wateja kimekuwa kikifanya kazi kwa bidii na hiyo yote inatokana na wateja kuongezeka kila kukicha. Hivyo basi kwa sasa kimeboreshwa zaidi na pia ningependa kuwataka nyinyi mawakala wetu muwe mnatoa huduma hii pia kwani ninaamini kuna maswali hata nyinyi mnaweza kuwasaidia. Ninawaomba muwe mnawapatia maelekezo mazuri zaidi ili waweze kuelewa huduma zetu.” Alihitimisha meneja huyo wa mauzo
Hafla hiyo fupi iliweza kuangazia masuala mbalimbali yahusuyo bidhaa na huduma mbalimbali zikiwemo chaneli na vipindi vinavyopatikana kwenye kisimbuzi cha StarTimes.
Kwa upande wake Meneja Masoko kitengo cha chaneli na vipindi vya StarTimes Tanzania, Bi. Paulina Kimweri alipata fursa ya kuwaelezea kwa kina mbali na kisimbuzi mawakala hao pia yawapasa kunadi na kile kilichomo ndani yake.
“Mimi kwa upande wangu ningependa kutoa wito kwenu nyinyi mawakala wetu kuwa inabidi muwe mnatoa elimu ya kutosha juu ya chaneli na vipindi vinavyopatikana kwenye visimbuzi vyetu. Kwani sio wateja wote ambao wana ufahamu na chaneli na vipindi vyetu. Wengi hununua bidhaa zetu kwa ajili ya kutazama chaneli na vipindi vya ndani tu bila ya kujua kuwa vipo vitu vingi vya kuvutia na kumfaa kila mtu ndani ya familia.” Alifafanua Bi. Kimweri
“Muwe mnawaambia wateja kuwa pia kuna chaneli nyingi tu za kuvutia ambazo zinapatikana katika vifurushi vya bei nafuu. Kwa mfano chaneli za watoto zenye vipindi vinavyofundisha, dini, filamu, tamthiliya, muziki, michezo, mitindo, makala nakadhalika,” alisema na kumalizia Bi. Kimweri, “Hivyo basi naamini kuwa mkitoka hapa mkirudi madukani mwenu mtakuwa mkivitumia vipeperushi tunavyowapatia kuwaelimisha wateja waweze kufahamu zaidi.”
StarTimes Tanzania mpaka hivi sasa ina mawakala wakubwa na wadogo zaidi ya 500 waliosambaa nchi nzima kuhukikisha inawafikia wateja kwa urahisi. Hivyo imewataka mawakala wote nchini kuwa waaminifu na pia wateja kuwatembelea kwani huduma wanazozitoa ni sawa na zile zinazotolewa katika ofisi za kampuni.
Kampuni inajivunia uwepo wa mawakala hao ambao kwa muda mrefu wamekuwa ni kiungo muhimu baina yao na wateja. Lakini kwa upande mwingine hii ni fursa kwa watanzania kuchangamkia fursa hii kwa kujiajiri wenyewe kwani kupitia uwakala mtu anaweza kuuza bidhaa na kupata kamisheni yenye faida kubwa na kuendesha maisha yake.
Post a Comment