KATIBU MKUU WA CCM, KOMREDI ABDULRAHMAN KINANA AUNGURUMA KARAGWE
- Afungua ofisi ya Saccos ya Vijana wa CCM
- Akabidhi pikipiki tano
- Asisitiza kuimarisha Chama cha Mapinduzi
- Ameahidi kusimamia haki na kutetea wanyonge
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Kihanga waliojitokeza kwa wingi kuwapokea yeye na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia mizinga ya nyuki kwenye mradi wa ufugaji nyuki Kishoju,wilayani Karagwe.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya namna ya ufugaji nyuki kisasa kutoka kwa moja ya viongozi wa mradi wa ufugaji nyuki na utunzaji wa mazingira Bw. David Kamala, Kishoju,wilayani Karagwe.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa banda maalum la kuzalishia malkia wa nyuki kwenye mradi wa ufugaji nyuki na utunzaji mazingira, Kishoju,wilayani Karagwe.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza mara baada ya kupokea taarifa za maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Kyaka -Bugene yenye urefu wa kilometa kwa kiwango cha lami.
Katibu Mkuu wa CCM yupo kwenye ziara mkoani Kagera akikagua, kusimamia na kuhimiza utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM.
Ujenzi ukiendelea kwenye barabara ya Kyaka kwenda Bugene yenye urefu wa kilometa 59.
Katibu Mkuu wa CCM akiteremka kwa kukimbia mara baada ya kukagua maendeleoa ya ujenzi wa barabara ya Kyaka kwenda Bugene yenye urefu wa kilometa 59.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa darasa la shule ya msingi Katembe,iliyopo katika kata ya Kituntu wilayani Karagwe.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na viongozi wa CCM wilaya ya Karagwe kuelekea kwenye eneo la mkutano kuwasalimia wananchi wa Katembe, kata ya Kituntu wilaya ya Karagwe mkoani Kagera.
Wakazi wa Katembe wakipunga mkono kama ishara ya kuusalimu msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye akiwasalimu wananchi wa Katembe kata ya Kituntu wilaya ya Karagwe.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimwambia jambo kwa msisitizo mbunge wa jimbo la Karagwe Gosbert Blandes mara baada ya kumaliza kuwasalimia wananchi wa kijiji cha Katembe,kata ya Kituntu wilaya ya Karagwe.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa kiwanda cha kukoboa Kahawa KADERES kilichopo kijiji cha Ndama kata ya Ndama wilaya ya Karagwe.
Ujenzi ukiendelea wa kiwanda cha kukoboa Kahawa KADERES kilichopo kijiji cha Ndama kata ya Ndama wilaya ya Karagwe.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Ubora na Viwango vya Kahawa Olwos-Kumu Roy alipotembelea kiwanda cha KADERES,Ndama wilaya ya Karagwe.
Haya ndio mapokezi ya Kinana kwenye kijiji cha Nyakaiga kata ya Kibondo wilaya ya Karagwe.
Mbunge wa Jimbo la Karagwe Gosbert Blandes akihutubia wakazi wa kijiji cha Nyakaiga kata ya Kibondo .
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa Nyakaiga kata ya Kibondo wilaya ya Karagwe mkoani Kagera na kuwaambia kuwa Wapinzani wameshapotezana na CCM inaendelea kuongoza hivyo kuwataka wananchi wa hapo wasibabaishwe.
Wananchi wa Nyakaiga wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Nyakaiga kata ya Kibondo ambapo alisisitiza CCM chini yake itasimamia haki na kuwatetea wanyonge.
Wakazi wa Nyaishozi wakifurahia ujio wa Kinana.
Wakazi wa kijiji cha Nyaishozi wilaya ya Karagwe wakifurahia ujio wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Nyaishozi wilayani Karagwe.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kufungua Saccoss ya Vijana wa CCM wilaya ya Karagwe.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisaini kitabu mara baada ya kufungua ofisi ya Saccoss ya Vijana wa CCM Karagwe, aliyesimama mbele yake ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM Ndugu Yahya Katembe.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa na Vijana watano waliowezeshwa boda boda na Saccoss ya Vijana Karagwe.
Vijana hao wameingia kwenye mpango maalum wa kuwawzesha vijana kumiliki boda boda zao.
Katibu Mkuu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiagana na wananchi waliokuja kushuhudia ufunguzi wa ofisi ya Saccoss ya Vijana.
Mbunge wa Jimbo la Karagwe Mhe. Gosbert Blandes akihutubia wananchi kwenye uwanja wa mkutano Kayanga.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ambapo aliwaambia wananchi hao CCM inaendelea kuwa chama pekee kinachojali wananchi na kusimamia maendeleo kwa kuwa na sera zinazotekelezeka.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Kayanga wilaya ya Karagwe mkoani Kagera ambapo aliwaambia wananchi hao zaidi ya vijiji 51 vitapata umeme .
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Kayanga, wilayani Karagwe.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye picha ya pamoaja na wanajeshi wenzake aliokuwa nao Monduli mara baada ya kuhutubia wananchi Kayanga wilaya ya Karagwe mkoani Kagera.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Post a Comment