KAMISHNA WA SENSA, HAJJAT AMINA MRISHO SAID ATANGAZA NIA YA UBUNGE JIMBO LA KITETO
Kamishna
wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 Hajjat Amina Mrisho Said akizungumza
na waandishi wa habari leo kuhusu nia yake ya kugombea nafasi ya Ubunge wa
Jimbo la Kiteto lililoko mkoani Manyara kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi
(CCM).
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi
ya mwaka 2012 Hajjat Amina Mrisho Said wakati akitangaza nia yake ya kugombea nafasi ya Ubunge wa Jimbo
la Kiteto lililoko mkoani Manyara kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Na
Mwandishi wetu
Kamishna wa Sensa ya
Watu na Makazi ya mwaka 2012 Hajjat Amina Mrisho Said ametangaza nia ya
kugombea nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Kiteto lililoko mkoani Manyara kwa tiketi
ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza na
waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Hajjat Amina Mrisho Said amesema iwapo
atateuliwa na CCM kuwa mgombea wa Jimbo la Kiteto, atahakikisha anatoa
ushirikiano wa hali ya juu ili kuleta maendeleo ya wananchi wa jimbo hilo.
Ametaja vipaumbele
vyake kuwa ni kufuatilia kwa ukaribu utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015 –
2020 na kufanikisha ujenzi wa Chuo cha VETA jimboni ili vijana waweze kupata
elimu ya stadi za kazi na hatimaye waweze kujiajiri.
Kuhusu suala zima la
ufugaji, Hajjat Amina amesema atahamasisha uendelezaji wa ufugaji wenye tija
kwa kuifuatilia Serikali ili iweke miundombinu katika maeneo yote ya wafugaji
jimboni.
Vipaumbele vingine ni
pamoja na kuhamasisha ujenzi wa Soko la Kimataifa la Mazao hasa mahindi ikiwa
ni pamoja na kutoa elimu ya matumizi ya stakabadhi ya mazao gharani na kuwashirikisha
wananchi wote katika kujiletea maendeleo kwenye maeneo yao.
Hajjat Amina Mrisho
Said kitaaluma ana Shahada ya Uzamili wa Mifumo ya Kompyuta na amewahi kuwa
Mkuu wa mkoa wa Iringa na Pwani ambapo kwa sasa ni Kamishna wa Sensa ya Watu na
Makazi ya mwaka 2012.
Post a Comment