Makamu mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MOI Prof Bakari Lembariti akihutubia wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa MOI wakati wa Uzinduzi wa Kikao cha Tatu cha Baraza Hilo. .....................................
Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya
Wadhamini ya MOI Profesa Bakari Lembariti leo amezindua vikao vya Baraza la
Tatu la Wafanyakazi wa MOI katika ukumbi wa IDDI NYUNDO katika halmashauri ya
Temeke jijini Dar es Salaam. Vikao vimehudhuriwa na zaidi ya wajumbe 50 kutoka
katika kila idara, vitengo na chama cha wafanyakazi wa MOI (TUGHE) na wajumbe
wa TUGHE mkoa.
Akizindua Baraza hilo Profesa
Lembariti alisema anampongeza Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt
John Pombe Magufuli. Alisema " Kwa
niaba ya Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini MOI Mh Zakia Meghji natumia Fursa hii kumshukuru
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa uongozi
wake uliotukuka na jitihada zake za kuboresha huduma za afya hapa nchini, sote
ni mashahidi".
Aidha, Profesa Lembariti
aliwakumbusha wafanyakazi wa MOI kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia maadili
ya utumishi wa Umma ili kujenga imani kwa watanzania walio wengi ambao
wanaitegemea MOI kama Taasisi pekee inayotoa Tiba ya kiwango cha juu cha rufaa
kwenye Tiba ya Mifupa, upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu.
Kwa upande wake ,akiwasilisha
ripoti ya utendaji wa Taasisi ya Kaimu Mkurugenzi wa MOI Dkt Othman Kiloloma
alisema kutokana na ongezeko kubwa la ajali ambazo zimepelekea ongezeko kubwa
la wagonjwa MOI, Taasisi ya MOI iko kwenye mpango mkakati kabambe wa
kushirikiana na baadhi ya hospitali za rufaa za pembezoni kwa kuwapeleka
wataalamu kutoa huduma katika hospitali hizo na kupunguza kama si kuondoa kabisa
wimbi la wagonjwa wanaopokelewa MOI.
|
Post a Comment