Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na watumishi wa Wizara yake wakati wa ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi la Wizara katika kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Desemba 08, 2016. .........................................
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amewataka watendaji na watumishi wa Wizara yake kuzingatia maadili na uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu yao.
Ameyasema hayo wakati akifungua Baraza la wafanyakazi la Wizara yake na kusisitiza kwa watendaji kuwasimamia watumishi walio chini yao kuzingatia maadili na uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu yao katika kutoa huduma kwa wananchi.
Ameongeza kuwa kuwepo kwa ushirikiano kati ya uongozi na watumishi utasaidia kufanikisha masuala mbalimbali ya maendeleo ya Wizara, Taasisi zake na watumishi katika kuleta maendeleo ya Wizara katika kutimiza wajibu wao.
“Nawataka watumishi wazingatie maadili katika kutekeleza wajibu wao na naamini kwa juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano tutarudisha maadili ya Utumishi wa Umma na bado taratibu zinaendelea kusimamiwa ipasavyo”asisitiza Mhe Nnauye.
Mhe. Nnauye amesisitiza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli ana mpango wa dhati wa kurujesha maadili katika Utumishi wa Umma na kuhakikisha heshima yake inarudi.
|
Post a Comment