Header Ads

Taasisi ya African Relief yaanzisha Kilimo cha Umwagiliaji Kijiji cha CHUMBI

Mkurugenzi wa Taasisi ya African Relief Organization, Samy  Mohammed Elazeb (kulia) akisimamia trekta likilima shamba lenye ukubwa wa ekali 2500 eneo la Khanga, katika Kijiji cha Chumbi C, wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani mwishoni mwa wiki,Taasisi hiyo itaanza uzalishaji wa mazao ya mahindi na mpunga.

  Mwenyekiti wa Taasisi ya African Relief Organization, Abdallah Ndauka akisimamia trekta likilima shamba lenye ukubwa wa ekali 2500 eneo la Khanga, katika Kijiji cha Chumbi C, wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani mwishoni mwa wiki.

 Ndauka akizungumza na vyombo vya habari kuhusu mradi huo.

 Vibarua akifyeka vichaka kusafisha shamba hilo.

 Mwenyekiti wa Taasisi ya African Relief Organization, Abdallah Ndauka na Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Samy  Mohammed Elazeb (kulia) wakisimamia trekta likilima shamba lenye ukubwa wa ekali 2500 eneo la Khanga, katika Kijiji cha Chumbi C, wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani mwishoni mwa wiki,Taasisi hiyo itaanza uzalishaji wa mazao ya mahindi na mpunga.

 Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Samy  Mohammed Elazeb akisimamia maandalizi ya shamba hilo.

 Ndauka na Samy  Mohammed Elazeb wakijadiliana jambo.

 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kijiji cha Chumbi C, Utete, wilayani Rufiji,mkoani Pwani, akielezea mbele ya wanahabari kijijini hapo mwishoni mwa wiki, jinsi Kijiji hicho, kilivyonufaika na misaada mbalimbali iliyotolewa kwao na Taasisi ya African Relief Organization. Kijiji hicho kimepatiwa misaada ya kisima cha maji, ukumbi wa mikutano, majengo ya ofisi na ukarabati wa shule ya Chumbi.

 Samy  Mohammed Elazeb (kushoto),  na mwanakijiji wakiziba maji kwenye mabomba ya kisima kilitolewa msaada na taasisi hiyo kwa Kijiji cha Chumbi C.


 Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Chumbi C, akikinga maji kwa mkono katika kisima hicho.

No comments

Powered by Blogger.