Header Ads

Bohari ya Dawa yazindua Mpango wa Huduma kwa Wateja Maalum Jijini Dar es Salaam


Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee naWatoto Dk. Mpoki Ulisubisya (kulia), akizungumza na viongozi mbalimbali wa sekta ya afya wakati akizindua mpango wa huduma maalumu kwa wateja wakubwa Dar es Salaam leo asubuhi.
............................................


Na Dotto Mwaibale

BOHARI  ya dawa (MSD) imezindua mpango wa huduma maalumu kwa wateja wake wakubwa, kama moja ya hatua za kuboresha huduma kwa wateja. 


Mpango huo utawawezesha wateja hao kupata huduma ya haraka zaidi pindi wanapokuwa wanahitaji mahitaji yao.


Wateja hao ni pamoja na hosipitali ya Taifa ya Muhimbili, Taasisi ya Mifupa (MOI), Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, hosipitali ya Sekoutoure Mwanza, Hosipitali ya Kibong’oto, Mirembe, Hosipitaliza Amana, Temeke, Mwananyamala, KCMC, Hospitaliya Benjamin Mkapa na Taasisi ya Moyo ya JakayaKikwete.


Akizindua mpango huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee naWatoto Dk. Mpoki Ulisubisya amesema mpango huo ni moja ya maboresho yanayofanywa na MSD, ili kuhakikisha huduma zake zinatolewa kama inavyohitajika.


Dk. Mpoki pia amewasisitiza wateja hao wakubwa wa MSD kuhakikisha wanafanya maoteo sahihi ya mahitaji yao na kuyaleta MSD kwa wakati ilikuepusha ucheleweshwaji wa taratibu za manunuzi ambao pia itasababisha dosari kwenye upatikanaji wa dawa kwa wateja. 


Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu  amesema hatua ya kuwahudumia wateja hao kwa kiwango kizuri na cha uhakika itafanikiwa, hivyo Watarajie maboresho makubwa ya huduma. 

Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)  Profesa Mohamed Janabi (kushoto), akizungumza katika hafla hiyo. 


Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu akizungumza kwenye mkutano huo.

Meneja Huduma kwa Wateja wa MSD, Salome Malamia akizungumza katika hafla hiyo.

Mmoja wa maofisa kutoka Ofisi ya Inayosimamia Utekelezaji wa Mapendekezo ya Maboresho (SMO), Naomi Shangani akitoa maelezo kwa mgeni rasmi kuhusu mpango huo.

Ofisa wa SMO, Frankie Nkone akieleza kazi za eneo lake zinavyofanyika.

Wajumbe wa mkutano huo kutoka sekta ya afya wakiwa wameinamisha vichwa vyao kwa dakika moja kumkumbuka aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya MSD, marehemu Profesa Idrissa Mtulia aliyefariki jana.

No comments

Powered by Blogger.