Watumishi Wawili wa Serikali Watimuliwa Kazi Wilayani ILEJE
Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Ileje, Haji Mnasi akiongea wakati wa kikao cha
Baraza la Madiwani.
Sehemu ya Wajumbe wa Baraza
la madiwani Wilaya ya Ileje.
na fredy mgunda,Ileje
BARAZA la Madiwani Wilayani
Ileje limebariki kufutwa kazi kwa watumishi wawili wa Halmashauri hiyo
kutokanana makosa ya wizi wa
mamillioni ya fedha za wafadhili za mradi wa UKIMWI wa water reed.
Akizungumza wakati wa
kufungwa kwa Baraza hilo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Ubatizo
Songa amesema kuwa, wameamua kuchukua uamuzi huo mara baada ya kuridhishwa na
uchunguzi uliofanywa na kamati ya uchunguzi
iliyoundwa na Ras wa Songwe na kubaini kuwa, Mganga Daraja la
pili Josephat Yisuya na Grace Kibona wameweza kuingizia Halamashauri hasara ya
zaidi Milioni 84.
“Josephati aliweza kujipatia
kiasi cha fedha shilingi milioni 36254200 /-wakati Grace Kibona Mhasibu Daraja
la kwanza aliweza kujipatia Kiasi cha shilingi milioni 48742500/-fedha za mradi
wa Water Aid zilizofika katika Halmashauri ya wilaya ya Ileje”alisema Songa.
Mwenyekiti huyo ameagiza
watu hao kurudisha kiasi hicho chote cha Fedha katika Akaunti ya Halmashauri
hili ziweze kufanya kazi zingine.
kwa mtumishi mwengine Anna
mwakipesile kesi yake bado inaendelea na uchunguzi wakati huo watumishi 2 baada
ya kamati ya uchunguzi iliyoundwa na ras songwe waliachiwa huru na kurudishwa
kazini baada ya tume kuridhika na utetezi wao.
Wakati huo huo Mkurugenzi
mtendaji Bw Haji Mnasi amewavua vyeo wakuu wa shule wawili ambao ni Henry Musomba
wa sekondari Ibaba na Emecka Minga wa sekondari Ngulugulu kwa makosa mabalimbali
yakiwemo utoro,uzembe ,lugha chafu na matumizi mabaya ralislimali.
Aidha Mnasi alisema kuwa ni
wakati wa kila mfanyakazi wa serikalini kujitathimni kwa kile alichofanya kwani
waliotuhumiwa ni wengi lakini bado uchunguzi unaendelea hivyo hawajaishia hapo
kwani kila mmoja atakayebainika kufanya ubadhilifu sheria itafata mkondo wake.
Ametoa onyo kwa watumishi
kuacha kujihusiha na mambo yaliyo kinyume na maadili ya utumishi wa kwa
kujiingiza katika masuala ya kifisadi serikali aitamfumbiamcaho kwani hu ni
wakatii wa kuwahudumia wananchi wa nyonge kwa maslahii ya Taifa.
“Mimi sipo tayari kufukuzwa
kazi kwa uzembe wa watumishi wazembe nitafuatili utendaji wa watumishi wote wa
Ileje ili tuweze kuwatumikia wananchi kama inavyopaswa na kuidumisha kauli ya
hapa kazi tu iliyotelwa na rais wetu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh Dr
John Pombe Magufuli” alisema Mnasi .
Post a Comment