Header Ads

Naibu Waziri SELEMAN JAFO awataka Maafisa Elimu Kutatua Kero za Walimu

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI  Selemani Jafo akisaini kitabu cha wageni shule ya sekondari Segera, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. Wiliam Makufwe na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe.

......................................................
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),SelemanI Jafo amewataka maafisa elimu kupanga muda wa kusikiliza kero za walimu na kuzitafutia ufumbuzi ili kuongeza morali ya walimu kufundisha.

Jafo ametoa agizo hilo alipokuwa akiongea na walimu wa shule ya sekondari Segera iliyopo wilayani Handeni, katika ziara yake aliyoifanya Wilayani Handeni na Mkoa wa Tanga. 

Amesema wapo baadhi ya Maafisa elimu ambao wanajifanya kuwa ni Miungu watu linapokuja suala la kusikiliza na kutatua kero za walimu.


“Najua wapo wapo walimu wanaotembea umbali mrefu kufuata huduma makao makuu ya Halmashauri kwa wakubwa wao mara nyingi wameshindwa kutatuliwa kero zao hali inayopelekea usumbufu, Kuanzia leo napiga marufuku tabia hiyo,”amesema Jafo. 

Amesisitiza Maafisa elimu hao wapo kwa lengo la kuwasikiliza walimu na kuwasaidia kutatua kero zao ili waweze kujikita katika ufundishaji wa wanafunzi. 

Kadhalika, amebainisha walimu ni watu muhimu sana nchini ila wamekuwa wakikatishwa tamaa na utendaji wa baadhi ya maafisa elimu. 

Viongozi wakisikiliza kwa makini maagizo ya Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Selemani Jafo.

Baadhi ya watumishi wa halmashauri ya Handeni.

No comments

Powered by Blogger.