Header Ads

SELEMANI JAFO awakomalia Wahandisi wa Halmashauri za mkoa wa TANGA


Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akizungumza katika kikao cha watumishi wilaya ya Handeni.
Watumishi wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo katika ziara yake aliyoifanya mkoani Tanga.

.........................................

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo amehitimisha ziara yake Mkoani Tanga huku akionesha kuchukizwa na kitendo cha Wahandisi wa ujenzi Katika Halmashauri za mkoa huo kwa kutozingatia mahitaji ya wanafunzi wenye ulemavu.

Jafo alifanikisha ziara yake ya siku tatu kwa kutembelea Halmashauri zote za mkoa wa Tanga.

Katika ziara yake mkoani huo, Jafo alikagua ujenzi wa vyoo vinavyo jengwa katika shule mbalimbali za sekondari mkoani Tanga kupitia mradi wa SEDEP II.

Akizungumza mara baada ya ziara yake, Jafo alisema amegundua vyoo vyote vilivyo kamilika na vinavyo endelea kukamikishwa mkoani huo havijazingatia kuweka miundombinu ya watu wenye ulemavu.

“Katika kila shule niliyopita nimekuta vyoo vizuri sana vimejengwa lakini vina kasoro ya kukosa hata tundu moja kwa maeneo yote ya wasichana na wavulana yaliyo andaliwa kwaajili ya watoto walemavu,”alisema Jafo.

Aliwaagiza wakurugenzi wote kuhakikisha hitaji hilo la msingi kwa watoto walemavu linazingatiwa kwa kufanya marekebisho kwa upande wa vyoo vya wavulana na wasichana ili kupata tundu moja kwa lengo la kuwasaidia watoto wenye ulemavu.

Jafo mara baada ya kuhitimisha ziara yake mkoani Tanga anaelekea kuanza ziara nyingine katika mkoa wa Ruvuma, Mtwara, Lindi na Pwani.

No comments

Powered by Blogger.