Header Ads

Rais Dkt MAGUFULI apokea Marais wa CHAD na ZAMBIA Jijini Dar es Salaam

 Rais wa Jamhuri ya Chad Mhe Idriss Deby Itno akipokea shada ya maua  mara  baada ya kiongozi huyo kuwasili katika uwanja wa  ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jioni ya leo Novemba 27, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake  Rais wa Jamhuri ya Chad Mhe Idriss Deby Itno mara  baada ya kiongozi huyo kuwasili katika uwanja wa  ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jioni ya leo. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake  Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu wakisimama kwa ajili ya nyimbo za Taifa na mizinga 11 mara  baada ya kiongozi huyo kuwasili katika uwanja wa  ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jioni ya leo Novemba 27, 2016.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt John Pombe Magufuli akimtambulisha Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu kwa Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe kassim Majaliwa baada ya kuwasili katika uwanja wa  ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jioni ya leo.

No comments

Powered by Blogger.