Header Ads

Madiwani MERU wamkataa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo

 Makamu mwenyekiti wa baraza la madiwani Meru akiwa anachangia hoja katika baraza hilo.

...........................................................


N Woinde Shizza, Arusha

Baraza la madiwani  Halmashauri ya Meru mkoani Arusha wamkaanga Mkurugenzi wasema hana uwezo wa kuongoza  Halmashauri hiyo.

Akitoa  maazimio  ya kikao  cha baraza kilichokaa siku mbili kilichowajumuisha  madiwani,wakuu wa idara mbalimbali na wataalam Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Willy Njau Alisema wametafakari kwa kina utendaji wa Mkurugenzi na kubaini kuwa hafai.

" Tumejadili ajenda ya utendaji  usioridhisha wa Mkurugenzi wetu na tumeona  kuwa haufai kutokana na mambo mengi anayoyafanya yanakiuka kanuni na taratibu za Halmashauri"alisema Njau.

Aliongeza kuwa Mkurugenzi huyo ameshindwa kukusanya makusanyo ya pesa kiasi cha milioni 150 kilichokusudiwa kukusanywa  tangu  Julai hadi septemba mwaka huu jambo alilosema linaweza kusababisha Halmashauri kutopewa ruzuku kutoka serikali kwasababu  ya uzembe.

" Tumejiridhisha kuwa uwezo wa Mkurugenzi kuiongoza Halmashauri yetu kama Mkurugenzi Mtendaji ni mdogo hivyo hafai anadidimiza maendeleo ya Halmashauri ya meru" alisema Njau. Na kuongeza.

"Tumeamua kuiomba mamlaka yake  na Uteuzi ichukue  hatua stahiki za kumuwajibisha ili kunusuru maendeleo ya Halmashauri ya meru".

Kwa upande wake mkurugenzi  Huyo Christopher Kazer  alisema anafuata maagizo ya mkuu wa nchi na hawezi kuwanyima watu kufikiri  wanavyofikiri.

" Maelekezo ya kupunguza matumizi yasiyolazima kutoka kwa mkuu wa nchi ninayafuata pia ndio maana nimepunguza matumizi mengi" alisema.

Alisema hawezi kuzuia maamuzi yanayotolewa na baraza hilo maana kwa namna moja au nyingine wamekaa wakatengeneza maamuzi hivyo hawezi kuwalazimisha kutofanya maamuzi.

Aidha pia alibainisha kuwa anaamini kabisa madiwani hawa wanataka halmashauri iendeshe kisiasa wanataka iendeshwe kama wao wanavyotaka kitu ambacho hatakubali kwani sio hakutumwa kufanya kazi ya siasa bali alitumwa kufanya kazi ya kuwasaidia wananchi na serikali kwa ujumla 

"ivi jamani ndugu waandishi mtu anatoka apo usa anataka alipwe nauli elfu 80 ni haki kweli wengine wanatoka apa apa wakija kikao kikichelewa kuisha wanataka walipwe  fedha za kulala laki laki sasa mimi hayo yote tumeyatoa sasa ivi wanalipwa elfu 40 tu na mshahara wao upo pale pale sasa wao ndio maana wananipiga zwegwe mimi nasema nitasimamia ilani ya chama ambacho kinaongoza serikali pia nitafata sera ya muheshimiwa Rais ya kubana matumizi sitakubali  wafanye vitu ovyo na ninyamaze walifikia atua wakataka hata kunigombanisha na watendaji wangu ila mimi nimeajiriwa na serikali mimi sio mwanasiasa na nitafanya kazi kama nilivyoaaidi siku nilioapishwa "alisema mkurugenzi  Kazer


 Baadhi ya madiwani wa meru wakifuatilia kikao.

 Mkurugenzi   wa halmashauri ya Meru  Christopher Kazer akifafanua jambo kwa waandishi mara baada ya baraza kumalizika.

  Mkurugenzi   wa halmashauri ya Meru  Christopher Kazer akijibu hoja mbele ya madiwani wa meru.

 Baadhi ya madiwani wakifuatilia.

No comments

Powered by Blogger.