Header Ads

Mhandisi RAMO MAKANI aongoza Siku ya Utundikaji Mizinga Kitaifa Mkoani PWANI

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani akizungumza na wananchi katika viwanja vya Mwambisi Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani jana wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kutundika Mizinga Kitaifa Mkoani humo. Naibu Waziri Makani ametoa wito kwa wananchi kutumia vizuri fursa ya maeneo ya misitu yaliyotengwa kwa shughuli za ufugaji nyuki kwenye ukanda wa wazi (buffer zone) kwa kutundika mizinga mingi na siyo kutumia maeneo hayo kwa shughuli nyingine za uharibifu wa mazingira kama uchomaji mkaa kwa kuwa kufanya hivyo kutasadia uhifadhi wa misitu na kuongeza uzalishaji bora wa mazao ya nyuki, Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu, Prof. Dos Santos Silayo (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Asumpta Mshana (wa pili kushoto).

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (katikati) akizindua Manzuki ya Makonga katika shamba la Miti Ruvu Kaskazini Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani jana wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kutundika Mizinga Kitaifa yaliyofanyika Wilayani humo. Manzuki hiyo itatumiwa kama shamba darasa la kuwaelimisha wananchi juu ya ufugaji wa nyuki kwa njia za kisasa zitakazowezesha kuzalisha mazao bora ya nyuki, Kulia ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Asumpta Mshana (wa pili kushoto) na Katibu Tawala Mkoa wa Pwani, Daniel Isala (kushoto).

 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (kulia) akitundika mzinga wa nyuki katika shamba la Miti Ruvu Kaskazini Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani jana wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kutundika Mizinga Kitaifa Wilayani humo, Kushoto anaeshiriki nae ni Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Asumpta Mshana na kushoto kwa Mkuu wa Wilaya ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Asumpta Mshana (kushoto) wakifunga mzinga wa nyuki baada ya kuutundika mapema jana katika shamba la miti Ruvu Kaskazini Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani.

 Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo (kulia) akitundika mzinga katika shamba la miti Mwakonga 2 Wilayani Kibaha jana. Prof. Silayo alisema kuwa kwa sasa Ofisi yake inasimamia jumla ya manzuki 92 zenye mizinga 7,129 ambazo zipo katika kanda 7 na mashamba ya miti manne. Aliongeza kuwa katika mwaka wa fedha 2015/2016 jula ya mizinga 2,706 ilivunwa na kupata asali kilo 7,129 za asali na kilo 195 za nta, Katika salamu zake Prof. Dos Santos alisema kuwa Asali ya Tanzania imepimwa katika maabara nchini ujerumani na kugundulika kuwa ni asali bora isiyo na kemikali na pia nyuki wa Tanzania hawana magonjwa hivyo asali yake ni salama, Alitoa wito kwa wananchi kutumia fursa zilizopo kufuga nyuki kwa wingi ili kujiinua kiuchumi na kuendeleza uhifadhi wa mazingira nchini.

(Na Hamza Temba - Wizara ya Maliasili na Utalii)



No comments

Powered by Blogger.