Header Ads

Waziri SIMBACHAWENE atembelea Banda la NEC kwenye Mkutano wa ALAT, Musoma

 Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  Bw.Kailima Ramadhani akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene kwenye banda la maonesho la Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakati wa mkutano wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) unaofanyika  mjini Musoma leo.
 Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  Bw. Kailima Ramadhani (kushoto), akimuelimisha mkazi wa Baruti mjini Musoma, Ismail Adudu alipotembelea banda la maonesho la Tume hiyo kwenye mkutano wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) mjini Musoma leo.Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Tume Emmanuel Kawishe, Naibu Katibu wa Idara ya Habari na Elimu kwa Umma, Giveness Aswile.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  Bw. Kailima Ramadhani(kushoto) akiwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Hamid M. Hamid (katikati) na Mjumbe wa Tume Mhe. Mchanga Mjaka wakiwa kwenye mkutano wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) mjini Musoma leo.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  Bw. Kailima Ramadhani (Kulia), akizungumza na Naibu Katibu wa Idara ya Habari na Elimu kwa Umma, Giveness Aswile (mbele yake) kwenye banda la maonesho la Tume hiyo wakati wa mkutano wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) mjini Musoma leo.Wengine ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Tume Emmanuel Kawishe, Afisa Habari Christina Njovu na Afisa Utumishi wa Tume Veronica Mollel.

No comments

Powered by Blogger.