Header Ads

TAMWA yataka Vyombo vya Habari Kutoa Fursa ya Wanawake Kusikika

Waandishi wa Habari kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa na Nyanda za Juu, wakiwa kwenye semina iliyofanyika Jumamosi wiki iliyopita Septemba 23, 2016 Jijini Dar es salaam. 

Semina hiyo iliandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA, ambapo pamoja na mambo mengine iliangazia kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuandika habari kuhusu mafanikio na changamo za wanawake ili kufanya jamii iwatambue na hivyo kuwafunguliwa fursa mpya ikiwemo kujitokeza kwenye masuala ya uongozi.

Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA, Alakok  Mayombo, akifungua semina hiyo.

Kushoto ni mkufunzi katika semina hiyo, Valerie Msoka ambaye ni Mkurugenzi wa Taasisi ya InterNews tawi la Tanzania. Pia ni Mkurugenzi mstaafu wa TAMWA.

Godfrida Jola ambaye ni Afisa Miradi TAMWA, akizungumza jambo kwenye semina hiyo.

Mshiriki..

Mshiriki kutoka Kanda ya Ziwa.

Vyombo vya habari nchini vimehimizwa kutoa fursa kwa wanawake kuonesha umahiri wa utendaji wao wa kazi ili kuleta chachu kwa wanawake wengi zaidi kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika jamii.

Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA, Alakok  Mayombo, alitoa rai hiyo jumamosi iliyopita kwenye mafunzo kwa wanaandishi wa habari kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa na Nyanda za Juu yaliyofanyika jijini dar es salaam.

Alisema bado idadi ya wanawake walio kwenye nafasi mbalimbali za uongozi serikalini ni chini ya asilimia 30 kwa nchi za kusini mwa Bara la Afrika ikiwemo Tanzania hivyo waandishi wa habari wana nafasi kubwa kuwahamasisha wanawake kujitokeza kuwania nafasi za uongozi.

Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo hayo ambayo yaliandaliwa na TAMWA, walisema mafunzo hayo yawatawasaidia kuandaa vipindi bora vitakavyowahamasisha wanawake nchini kujitokea kuwania nafasi za uongozi katika jamii.
                     

No comments

Powered by Blogger.