Header Ads

Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA mgeni Rasmi Kesho Uwanja wa Taifa

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw Alex Nkenyenge akifafanua kuhusu maandalizi ya Uwanja wa Taifa kwa ajili ya mechi ya kesho kati ya wabunge mashabiki wa Simba na Yanga Wasanii wa Bongo Flava na Bongo Movies itakayofanyika kesho.
Mwenyekiti wa Bunge Sports Club  Mhe. William Ngeleja akizungumza na waandishi wa Habari(hawapo pichani) kuhusu mechi ya kesho kati ya wabunge mashabiki wa Simba na Yanga na Wasanii wa Bongo Flava na Bongo Movies katika  Uwanja wa Taifa na kutangaza kuwa mgeni rasmi katika mechi hiyo atakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe Kassim Majaliwa.
Mwenyekiti wa Bunge Sports Club Mhe. William Ngeleja akionesha moja ya kikombe kwa waandishi wa Habari(hawapo pichani) kitakachotolewa kwa mshindi katika mechi ya kesho kati ya wabunge mashabiki wa Simba na Yanga na Wasanii wa Bongo Flava na Bongo Movies katika  Uwanja wa Taifa.
Mwakilishi wa wasanii wa Bongo Movie Bw.William Mtitu akizungumza kuhusu maandalizi ya timu yao kabla ya mchezo wao wa kesho na wasanii wa Bongo Flava utakaofanyika katika Uwanja wa Taifa kwa dhumuni la kuchangisha fedha kwaajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifatilia mkutano huo...

No comments

Powered by Blogger.