Header Ads

Serikali yaahidi Kuendeleza Mchezo wa HOCKEY hapa Nchini

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa naMichezo Mhe. Nape Moses Nnauye (katikati) akiangalia zawadi aliyopokea kutoka kwa Rais wa Shirikisho la Mchezo wa Mpira wa Magongo (Hockey)  Duniani Bw. Leandro Negre(Kushoto) mara baada ya kumaliza mazungumzo yaliyohusu maendeleo ya mchezo wa Hockey Tanzania kulia ni Rais wa Shirikisho la Mchezo wa Mpira wa Magongo (Hockey)  Afrika Bw. Seif Ahmed  Septemba 21,2016.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye(katikati) akizungumza na waandishi (hawapo Pichani) kuhusu ujio wa Rais wa Rais wa Shirikisho Mchezo wa Mpira wa Magongo (Hockey) Duniani kushirikiana na Tanzania kuendeleza mchezo wa Hockey Tanzania kulia ni Rais wa Shirikisho la  Mchezo wa Mpira wa Magongo (Hockey)  Duniani Bw. Leandro Negre na kushoto ni Rais wa Shirikisho la Mchezo wa Mpira wa Magongo (Hockey)  Afrika Bw. Seif Ahmed Septemba 21,2016
 Rais wa Shirikisho la Mchezo wa Mpira wa Magongo (Hockey)  Duniani Bw. Leandro Negre akizungumza na waandishi (hawapo Pichani) kuhusu ujio wake na mpingo yake ya  kushirikiana na Tanzania kuendeleza Mchezo wa Mpira wa Magongo (Hockey)  Tanzania kushoto ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye Septemba 21,2016.


Na Genofeva Matemu – WHUSM

Serikali ipo tayari kuendeleza michezo yote badala ya kubaki na michezo michache ikiwemo mchezo wa mpira wa magongo (Hockey) ambao kwa miaka mingi iliyopita mchezo huo uliiletea heshima kubwa Tanzania.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye wakati wa ziara ya marais wa shirikisho la Mchezo wa Mpira wa Magongo Duniani na Afrika leo Jijini Dar es Salaam.

“Mchezo wa mpira wa magongo ni mchezo ambao Tanzania kwa miaka mingi iliyopita ulituletea heshima kubwa hivyo kwa ujio ziara ya marais wa shirikisho la Mpira wa Magongo (Hockey) Duniani na Afrika itasaidia kuurejesha mchezo huo kwenye hadhi yake”, alisema Mhe. Nnauye.

Mhe. Nape Nnauye amesema kuwa Mchezo wa Mpira wa Magongo (Hockey) ni moja ya michezo ambayo inachezwa sana kwenye mishindano ya Olympic hivyo kama Tanzania itafanya maandalizi ya kutosha pengine Olympic ijayo ikapata fursa ya kuwa na wachezaji wa Hockey ambao watashiriki Olympic na kuiwezesha kupata medali za mchezo huo.

Naye Rais wa mchezo wa Mpira wa Magongo (Hockey) Duniani Bw. Leandro Negre ameahidi kusaidia miundombinu ya mchezo huo hasa uwanja kurejesha jitihada zinazofanywa na Tanzania huku akiiomba serikali kuipatia ardhi itakayowawezesha kujenga uwanja mzuri na wa kisasa kupitia shirikisho la mchezo wa mpira wa magongo duniani.

Aidha Rais wa Mchezo wa Mpira wa Magongo (Hockey) Afrika Bw. Seif Ahmed ameahidi kuongeza miundombinu katika uwanja wa kisasa utakaojengwa na shirikisho la mchezo wa mpira wa magongo duniani nchini Tanzania kwa kuuwekea miundombinu muhimu ikiwemo mataa na vitu vingine ili kuhakikisha uwanja huo unakua na hadhi ya kuchezwa michezo ya kimataifa.

No comments

Powered by Blogger.