Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA amesema Serikali Itaendelea Kusimamia Uchumi wa Nchini
Na Beatrice Lyimo, Dodoma
Serikali ya Jamhuri
ya muungano wa Tanzania inaendelea kukutana na wadau tofauti wanaohusika na
masuala ya uchumi katika kuhakikisha uchumi wa nchi unaendelea kukua.
Hayo yamesemwa na
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Hai Mhe.
Freeman Mbowe mijini Dodoma aliyetaka kujua hali ya uchumi ilivyo kwa sasa hapa
nchini.
Waziri Mkuu amesema kuwa lengo kuu la Serikali ya awamu
ya tano ni kuhakikisha uchumi wa nchi unaongezeka kupitia nyanja tofauti kwa
kushirikiana na taasisi za fedha zilizopo ili kufikia uchumi wa kati kama
ilivyoanishwa kwenye ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi.
Akizungumza kuhusu
suala la midororo wa upokeaji wa mizigo katika bandari nchini, Waziri Mkuu
amesema kuwa mdororo huo umetokana na kupungua kwa kiasi cha mizigo na kushuka kwa uchumi duniani.
Katika suala ya
mauaji yaliyotokea Tanga, Mwanza na Vikindu, Waziri Mkuu amesema kuwa usalama
wa wananchi utaendelea kuimarishwa huku serikali ikiahidi kupambana vitendo vya
mauaji kwa raia na askari katika maeneo mbali mbali nchini.
“Serikali imesikitika
sana na jambo hili la mauaji hivyo itahakikisha wauaji hao wanawekwa katika
mikono ya Sheria na kuongeza ulinzi kwa maeneo yote nchini kwa kuanzia ngazi ya
vitongoji” alifafanua Waziri Mkuu.
Mbali na hayo Waziri
Majaliwa ametoa wito kwa wananchi kushirikiana na vyombo vya dola katika
kuthibiti matukio hayo.
Kuhusu suala la uwepo
wa tozo katika zao la korosho swali limeibuliwa na Mbunge wa viti maalumu Mhe.Riziki
Lulida (CUF), Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa Serikali imeshatoa maelekezo
kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya kusimamia uondoaji wa Tozo zisizo na maana katika
zao la korosho.
Post a Comment