Header Ads

Taswira ya Leo Bungeni Mjini Dodoma

Baadhi ya Wabunge wakiingia katika ukumbi wa bunge kuhudhuria kikao cha 2 cha bunge la kumi na moja  la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mbunge wa Jimbo la Urambo Mhe.Margaret Sitta akimueleza Jambo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa leo Mjini Dodoma.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (MB) akimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba Leo Bungeni Mjini Dodoma.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kintinku  mkoni Singida wakifuatili vikao vya Bunge leo Mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akijibu swali wakati wa kikao cha 2 cha bunge la Jmahuri ya Muungano wa Tanzania ambapo alisema serikali haina mgogoro wowote wa mafuta baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar leo Mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bunge Mhe. Andrew Chenge akiongoza kikao cha Bunge leo Mjini Dodoma.

No comments

Powered by Blogger.