Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen
Gaudence Milanzi akikabidhi rasmi hati
kwa kiongozi wa Jumuiya ya
Uhifadhi wa Wanyamapori ya JUHIWANGUMWA Bw. Shaban Dinongo ya kuitambua
Jumuiya hiyo kama chombo halali
kilichosajiliwa kisheria kwa ajili ya
kusimamia rasilimali za wanyamapori zilizopo ndani ya eneo laJumuiya
hiyo kwa tangazo la serikali Na. 204. Makabidhiano
hayo yamefanyika jana katika kijiji cha
Utete Wilayani Rufiji
.................
Serikali kupitia Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen Gaudence Milanzi, imekabidhi rasmi
hati ya ya kuitambua Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya JUHIWANGUMWA kama
chombo halali kilichosajiliwa kisheria kwa ajili ya kusimamia
rasilimali za wanyamapori zilizopo ndani ya eneo la Jumuiya hiyo, Rufiji mkoani Pwani.
Pia, imekabidhi hati ya
matumizi endelevu ya rasilimali za Maliasili hususani wanyamapori kwa
kuwapa wananchi mamlaka ya kusimamia na kutumia rasilimali
hizo kwa kuwa na uhifadhi na maendeleo endelevu kwa faida ya kizazi
cha sasa na kijacho katika maeneo yao, Taifa na Dunia kwa ujumla.
Akizungumza jana katika kijiji cha Utete
wilayani Rufiji wakati akikabidhi hati
hizo mbili kwa pamoja kwa Jumuiya ya hifadhi ya wanyamapori ya
JUHIWANGUMWA , Milanzi amewatahadhalisha Viongozi wa Jumuiya hiyo kuwa
na waadilifu wawazi hususani katika masuala
ya pesa na mikataba watakayoingia na wawekezaji ili kuweza kuepuka migogoro
isiyo ya lazima kutoka kwa Wananchi ambayo imekuwa ikijitokeza mara
kwa mara katika jumuiya nyingine.
‘’Tunataka fedha zitakazopatikana kupitia utalii
wa Picha na utalii wa uwindaji ( photographic
and tourist hunting) zitumike katika huduma za kijamii kwa kuboresha miundombinu,
shule, hospitali na huduma nyinginezo za kijamii na sio pesa hizo zitumike
kuwaneemesha watu wachache’’ alisema Milanzi
Aliongeza kuwa, Serikali
kuu ( Wizara) itaendelea kuwasaidia pale inapohitajika kufanya hivyo katika
masuala ya Uhifadhi, ‘’hatutaki kuwaingilia katika
masuala yenu mfano katika masuala ya mapato na
matumizi hivyo nawataka mshirikiane na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ili
msiweze kutumbukia kwenye migogoro ya namna hiyo’’ alisisitiza Milanzi
Aidha , Maj.Gen. Milanzi
amewataka Wakuu wa Wilaya ya Rufiji, Malinyi, Kilombero
na Ulanga ambazo ni Wilaya zinazounda jumuiya hiyo ya
JUHIWANGUMWA yenye ukubwa wa kilomita za mraba 496.5 Kuhakikisha
kuwa wanashirikiana na wananchi kuzuia mifugo isiingie ndani
ya hifadhi kwa kuwa ni kinyume cha sheria ya uhifadhi kulisha mifugo
hifadhini.
Milanzi alisema ‘’ Suala
la kuingiza mifugo kwenye hifadhi lisiwe la kisiasa ni lazima kila
mwananchi atambue kuingiza mifugo ndani ya hifadhi ya wanyamapori ni kuvunja
sheria ya Uhifadhi hivyo atakayebainika lazima sheria ifuate mkondo wake’’
|
Post a Comment