Header Ads

Baraza la Michezo TANZANIA ( BMT ) latakiwa kuongeza Kasi ya Kufuatilia viwanja vya Michezo Vilivyovamiwa

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sana na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akipokelewa na Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohamed Kiganja alipofanya Ziara katik ofisi za Baraza hilo leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia ni mjumbe wa BMT Bibi. Jenifer Mmasi Shang’a na Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Makoye Alex Nkenyenge.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sana na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akizungumza na wafanyakazi wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) alipofanya Ziara katika ofisi za Baraza hilo leo jijini Dar es Salaam.

...............................
BMT yaagizwa kuongeza kasi ya ufuatiliaji wa viwanja vya michezo vilivyovamiwa nakuvirejesha kwa jamii kwa ajili ya matumizi ya michezo.

Agizo hilo limetolewa leo na na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nuru Khalifani Milao alipofanya ziara katika ofisi za Baraza hilo kwa ajili ya kujionea hali ya utendaji katika baraza hilo.

Mhe. Wambura alisema kuwa kumekuwa na changamoto ya maeneo mengi yaliyotengwa kwa shughuli za kijamii ikiwemo michezo kuvamiwa na watu na kufanya shughuli kinyume na taratibu.
“Kama ilivyo katika Ilani ya uchaguzi BMT mnawajibika kufuatilia maeneo yote yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli za michezo fuatilieni kwa karibu kikiwemo na kile cha Tandika ambacho tulikwisha anza nacho” Alisema Naibu Waziri.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sana na Michezo Bibi. Nuru Halfani Mrisho Milao akizungumza jambo wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa wizara hiyo Mhe. Annastazia James Wambura (katika) katika ofisi za Baraza la Taifa la Michezo leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa BMT Mohamed Kiganja.
Katibu Mkuu wa BMT Mohamed Kiganja akifafanua jambo mbele ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura (kushoto) alipofanya ziara katika ofisi za Baraza hilo leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Utumishi wa BMT Bw. Jacob Nduye na wapili kulia ni mjumbe wa BMT Bibi. Jenifer Mmasi Shang’a.

.................

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohamed Kiganja alisema kuwa pamoja na changamoto zilizopo watahakikisha wanapiga hatua katika kukuza sekta ya michezo kwani BMT ndiyo mkono pekee wenye dhamana ya kusimamia michezo kisheria.

Hata hivyo alielezea changamoto zinazowakabili katika kutekeleza majukumu yao kuwa ni kuwa ni ufinyu wa bajeti, upungufu wa wafanyakazi na muingiliano wa Wizara mbili katika utekelezaji katika ngazi ya Manispaa na Halmashauri Maafisa Michezo wanawajibika chini ya Wizara ya TAMISEMI hivyo kuna haja ya kukaa pamoja na kuangalia namna bora ya kushirikiana.

No comments

Powered by Blogger.