Header Ads

Mgombea Urais wa CCM, Dkt JOHN MAGUFULI aunguruma KISARAWE na UKONGA kabla ya Kuelekea ZANZIBAR

 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli akinyooshewa vidole gumba na wakazi wa Jimbo la Ukonga ikiwa ni ishara ya kukubali kumpigia kura ya ndiyo , wakati wa mkutano wa kampeni eneo la Moshi Bar, Ukonga Dar es Salaam. 

 Wakazi wa Mombasa, Ukonga, Dar es Salaam wakiuzuia msafara wa Dk Magufuli ulipokuwa ukitoka Kisarawe kwenda eneo Moshi Baa kuendelea na kampeni.

 Mmoja wa wakazi wa Mombasa, Ukonga akijitahidi kupiga Push Up mbele ya msafara wa Dk Magufuli.

 Wakazi wa Mombasa Ukonga Dar, wakifanya mazoezi ya Push Up mbele ya msafara wa Dk Magufuli.

 Dk Magufuli aiomba kura kwa wananchi wakati wa mkutano wa kampeni Jimbo la Ukonga, Dar es Salaam leo.

 Wafuasi wa CCM wakiongozwa na Agnes Ngonyani 9katikati) wakishangilia baada ya kufurahishwa na ahadi zilizokuwa zikitolewa na Dk Magufuli kwa wakazi wa Ukonga ikiwemo ujenzi wa Barabara ya Mombasa hadi Moshi Baa kwa kiwango cha Lami na Barabara ya njia sita kutoka Banana hadi Chamazi. 

 Dk Magufuli akimnadi Mgombea ubunge Jimbo la Ukonga kupitia CCM, Jerry Silaa wakati wa mkutano wa kampeni jimboni humo leo.

 Dk Magufuli akionesha kadi ya aliyekuwa Mkuu wa Red Brigade ya Chadema Ukonga ambaye aliirudisha na kuamua kuhamia CCM katika mkutano huo.

 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli akiagana na wakazi wa Jimbo la Ukonga baada ya kuhutubia  mkutano wa kampeni eneo la Moshi Bar, Ukonga Dar es Salaam.

 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli akiagana na wakazi wa Jimbo la Ukonga baada ya kuhutubia  mkutano wa kampeni eneo la Moshi Bar, Ukonga Dar es Salaam.

 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli aksalimiana na abiria eneo la Mombasa, alipokuwa anatoka katika   mkutano wa kampeni eneo la Moshi Bar, Ukonga Dar es Salaam.

 Wananchi wa Jimbo la Kisarawe, mkoani Pwani wakishangilia hotuba ya Dk Magufuli  wakati wa mkutano wa kampeni mjini Kisarawe leo.

Dk Magufuli akimnadi mgombea ubunge Jimbo la Kisarawe, Seleman Javo wakati wa mkutano wa kampeni mjini Kisarawe leo. 

No comments

Powered by Blogger.