Header Ads

Makamu wa Rais Dkt BILAL, amnadi MOHAMMED MGIMWA Jimbo la Mufindi Kaskazini

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. MOhammed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa Jimbo la Mufindi Kaskazini, mkoani Iringa wakati wa mkutano wa Kampeni za mgombea Ubunge wa jimbo hilo, Mohamed Mgimwa.
Baadhi ya Vijana wa CCM wa Jimbo la Mufindi Kaskazini, wakiruka na kucheza staili ya mgombea Urais kupitia CCM, John Magufuli, wakati wa mkutano wa kampeni za mgombea Ubunge wa jimbo hilo, Mohamed Mgimwa, zilizofanyika mwishoni mwa wiki, jimboni hapo.
Sehemu ya Wana CCM, waliojitokeza katika mkutano huo, wakimshangilia mgombea wao Mohammed Mgimwa wakati akitambulishwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya Viongozi wa Jimbo la Mufindi Kaskazini, Mkoani Iringa wakati alipowasili Jimboni hapo juzi Okt 17, 2015 kwaajili ya kumnadi mgombea Ubunge wa Jimbo hilo, Mohamed Mgimwa.

No comments

Powered by Blogger.