Header Ads

CCM yahitimisha Kampeni zake Jijini Mwanza

Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli akiwapungia  wananchi alipowasili kwenye mkutano wa kuhitimisha  kampeni kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza jana. Dk Magufuli amefanya kampeni nchi nzima kwa barabara kwa kusafiri kwa magari  zaidi  ya Km 40.

Dk Magufuli amewaomba watanzania wote kumpigia kura za ndiyo katika uchaguzi mkuu unaofanyika leo ambapo yeye amesema atawalipa kwa kufanya kazi kwa bidii ili kuwaletea maendeleo Wanzania.

Dk Magufuli akibusu kiganja chake ikiwa ni ishara ya kuwapenda wananchi waliofurika leo kwenye mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Kirumba, Mwanza.

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete (kulia), akimnadi Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli katika mkutano wa kuhitimisha  kampeni kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza jana. Dk Magufuli amefanya kampeni nchi nzima kwa barabara kwa kusafiri kwa magari zaidi  ya Km 40.

Rais Jakaya Kikwete akiwaomba watanzania kumpigia kura nyingi za ndiyo Dk Magufuli kwani anamuamini na atawachapia kazi na kulifanya Taifa lisonge mbele.

Wananchi wakishangilia baada ya kunogewa na ahadi lukuki alizozitoa Dk Magufuli kwa wakazi wa Mwanza na Kanda ya Ziwa na Tanzania kwa ujumla.

Ni furaha iliyoje kwa wakazi hawa wa Mwanza wakati wa mkutano huo wa kuhitimisha kampeni kwenye Uwanja wa CCM, Kirumba.

Yote haya yalikuwepo Kirumba.

Warembo wakisikiliza kwa makini wakati Rais Jnakaya Kikwete, ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Unsalama akitangaza kwamba uchaguzi utafanyika kwa uhuru na amani na kwamba wanaoota kufanya fujo watakiona cha moto.

Moja ya vionjo uwanjani hapo.

Rais Jakaya Kikwete akimnadi kwa wananchi mgombea ubunge Jimbo la Ilemela, Anjelina Mabula.

Rais Kikwete akimnadi kwa wananchi  mgombea ubunge Jimbo la Nyamagana kupitia CCM, Stanslaus Mabula.

Kweli HAPA KAZI TU Kwa Dkt MAGUFULI.

Malkia wa Mipasho, Khadija Kopa akitumbuiza wakati wa mkutano huo.

Ni furaha iliyojeDk Magufuli akiwasalimia wananchi.

Dk Magufuli akiwasalimia wananchi Uwanja wa Kirumba, jijini Mwanza.



Baadhi ya wasanii wa Kikundi cha Ngoma za asili cha Mchele mchele  wakifurahi baada ya Dk Magufuli kutangaza kuwasaidia wasanii endapo akishinda urais.

Dk Magufuli na Mratibu wa Kampeni za Dk Magufuli, Abdallah Bulembo pamoja na viongozi wengine akicheza kwa furaha wakisubiri kumpokea Rais Kikwete.

Dk Magufuli akiongozana na Rais Kikwete baada ya kumlaki Uwanjani hapo.

Dk Magufuli na Kikwete wakiwasalimia wananchi kwa kuwapungia mikono.

Msanii akiwa amejipamba kwa picha za Dk Magufuli na Mama Samia Suluhu Hassan.

Mgombea Mwenza Samia Suluhu Hassan akilakiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Anthony Diallo.

Mgombea Mwenza wa urais wa Tganzania kupitia CCM, Samia Suluhu Hassan akibadilisha mawazo na Mratibu wa kampeni za Magufuli, Abdallah Bulembo wakati wa mkutano wa kuhitimisha kampeni jijini Mwanza leo.

Yamoto Band ikitumbuiza wakati wa kampeni hizo.

Kila mmoja alinogewa na  muziki wa CCM uliokuwa ukiporomoshwa uwanjani hapo.

Dk Magufuli na Rais Kikwete wakicheza muziki uliokuwa ukiporomoshwa wakati wa kampeni jijini Mwanza leo.

Msanii JB akiwa na kundi la Team Kibajaj wakielezea jinsi wasnanii hao walivyofanikiwa  kuwashawishi watanzania kumpigia kura za ndiyo Dk Magufuli.


Msanii Fid Q akighani wimbo wa Hip Pop  w3a kuifagilia CCM na Dk Magufuli.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu nchini, akielezea jinsi walivyowashawishi vijana na wanavyuo kuipigia kura CCM na Dk Magufuli.

Shmrashamra zilivyokuwa uwanja hapo.

Moja ya mabango yaliyokuwepo Uwanjani hapo.

No comments

Powered by Blogger.