Header Ads

Dkt JOHN MAGUFULI ashiriki Mapokezi ya Mwili wa Dkt ABDALLAH KIGODA, Jijini Dar es Salaam

 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akizungumza na vyombo vya habari jinsi alivyomfahamu aliyekuwa waziri wa Viwanda na Biashara, marehemu Dk Abdallah Kigoda wakati wa mapokezi ya mwili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dcar es Salaam jioni hii, ukitokea India ambako alipatwa na mauti.

 Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, na Mgombea ubunge Jimbo la Handeni kupitia CCM, marahemu Dk Abdallah Kigoda, ukihamishiwa kwenye gari lingine wakati wa mapokezi ya mwili huo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam jana, ukitokea nchini India ambako alipatwa na mauti. 

Mwili huo ulikwenda kuhifadhiwa Hospitali ya Jeshi ya Lugalo, kusubiri kuagwa katika Ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam.

 Dk Magufuli akimfariji mtoto wa marehemu Dk Kigoda kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.

 Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha Rose Migiro akimfariji dada wa marehemu Dk Kigoda, Dk Aisha Kigoda.

 Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahiza akimfariji mjane wa marehemu Dk Kigoda, Rasul Kigoda.

 Dk Magufuli akizungumza jambo na Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue wakati wa mapokezi ya mwili wa marehemu Dk Kigoda Uwanja wa Ndege.

 Dk Magufuli akisalimiana na wananchi waliofika kuupokea mwili wa marehemu Dk Kigoda.

Dk Magufuli (kulia) akiangalia jeneza lenye mwili wa Dk Kigoda ukishushwa wakati wa mapokezi ya mwili huo kwenye Uwanja wa Ndege, Dar es Salaam.

No comments

Powered by Blogger.