Header Ads

Zoezi la Kuwapokea Wakimbizi Kutoka BURUNDI, Limeendelea Kambi ya Nyarugusu Mkoani KIGOMA

1
Mkuu wa kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu B iliyopo wilayani Kasulu Mkoani Kigoma, Fredrick Nisajile akiongea na wakimbizi walio katika mpango wa kuhamishiwa kwenye kambiza Nduta, Mtendeli na Karago.Wakimbizi hao waliopokelewa kutoka nchini Burundi hivikaribuni kwa sasa wanahifadhiwa kwa muda katika kambi ya Nyarugusu.

2
Wakimbizi kutoka nchini Burundi wakipanga mizigo yao katika kambi ya Nyarugusu wilayani Kasulu mkoani Kigoma ambapo wamehifadhi wa kwa muda kabla ya kuhamishiwa kwenye kambi za Nduta, Karago na Mtendeli ikiwa ni mkakati unaoratibiwa na Wizaraya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia Wakimbizi (UNHCR) na mashirika mengine ya kimataifa ili kuwapatia makazi salama.

3
Mtoto Jamine Nibetanga (14), kutoka nchini Burundi akiandaa chakula katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu B iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma ambapo wakimbizi kutoka nchini Burundi wanahifadhiwa kwa muda kabla ya kuhamishiwa kwenye kambizaNduta, KaragonaMtendeli.

4
Mkimbizi kutoka nchini Burundi, KukimanaDafroza (katikati), akifuma kikapu kama alivyokutwa katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu B iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma ambapo wakimbizi kutoka Burundi wanahifadhiwa kwa muda kabla ya kuhamishiwa katika kambi nyingine. Wengine ni Mkabanura Eviline (kushoto) na Niragira Dafroza (kulia).

5
Watoto wa wakimbizi kutoka nchini Burundi wakichota maji jana katika moja ya vituo vya maji vilivyowekwa katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu B iliyoko wilayani Kasulu Mkoani Kigoma ambapo wanahifadhiwa kwa muda. Wizaraya Mambo ya Ndani ya Nchi ina mpango wa kuwahamishiwa katika kambi za Karago, Mtendelina Nduta ili kupunguza msongamano uliopo katika Kambi ya Nyarugusu.

6
Mkimbizi kutoka nchini Burundi, Jacqueline Elulu (mwenye mtoto), akisubiri kupata huduma ya afya katika kituo cha Red Cross kinachotoa huduma za afya kwa wakimbizi walioko katika kambi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma. Shirika la Red Cross ni mojawapo ya wadau wanaoshirikiana na Serikali kutoa huduma za afya katika kambi ya Nyarugusu.

7
Mkimbizi Joseph Mtagura aliyeko katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu akiandaa mihogo yakuwauzia wakimbizi wenzake wanaoishi katika kambi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma.

8
Mkimbizi kutoka nchini Burundi, Ntirampeba Acquelina akianika mihogo ambayo huwauzia wenzake katika kambi ya Nyarugusu B iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma. Ugali wa mihogo ni mojawapo ya vyakula muhimu vinavyotumika katikakambi ya Nyarugusu.

9
Watoto wa wakimbizi kutoka nchini Burundi wanaohifadhiwa katika kambi ya Nyarugusu wakicheza mpira Wakimbizi hao wamekua wakiingia nchini kutokana na machafuko ya kisiasa yaliyotokea nchini Burundi hivi karibuni.

10
Wakimbizi kutoka Burundi walioko katika Kambi ya Nyarugusu wakiandaa mboga ya kisamvu. 

11
Mkimbizi Haverimana Ejide (kushoto) na mkewe Kugimana Evona pamoja na watoto wao wakipata chakula cha mchana katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu B iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma ambapo wanahifadhiwa kwa muda kabla ya kuhamishiwa maeneo mengine ili kupunguza msongamano uliopo katika kambi ya Nyarugusu.
 
(PICHA ZOTE NA  WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI)

No comments

Powered by Blogger.