Header Ads

Timu ya Taifa Yaelekea CONGO, Kwa ajili ya Michuano ya AFRIKA

x4
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Leonard Thadeo (kushoto) akimkabidhi mmoja wa wanariadha Bendera ya Taifa tayari kwa  safari yakuelekea nchini Congo Brazaville kwenye mashindano ya Afrika (All African Games), Timu hiyo iliondoka jana jioni na ndege ya Shirika  la Ndege la Tanzania. 

(Pichana Benjamin Sawe- WHVUM)

1x
Afisa Michezo Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Gordon Nsajigwa akimpatia mmoja wa wachezaji wa Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wanawake tiketi jana jioni tayari kwa safari yakuelekea Congo Brazaville kwenye mashindano ya Afrika (All African Games), kushoto aliyevaa sutini Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Leonard Thadeo.

x2
Wachezaji wa Timu ya Taifa wakipanda ndege ya Shirikia la Ndege la Tanzania (Air Tanzania) jana jioni tayari kwa kuanza safari ya kuelekea nchini Congo Brazaville kwaajili ya Mashindano ya Afrika (All African Games).

No comments

Powered by Blogger.