Header Ads

Makamu wa Dkt MOHAMMED BILAL, Afungua Kongamano la AFRIKA, Kuhusu Makubaliano ya Rasimu mpya ya Dunia

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Kongamano la Afrika kuhusu Makubaliano ya Rasimu mpya ya Dunia inayohusu Usimamizi wa Masuala ya Tabianchi, Kongamano hilo lilianza jana Sept 3, 2015 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mh.  Dianna Melrose, wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Afrika kuhusu Makubaliano ya Rasimu mpya ya Dunia inayohusu Usimamizi wa Masuala ya Tabianchi.    

Baadhi ya Washiriki wa Kongamano hilo wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akihutubia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo baada ya ufunguzi jana. Picha na OMR.

No comments

Powered by Blogger.