Header Ads

SOKO LA SINZA BUS TERMINAL LAZINDULIWA RASMI

1
Meya wa manispaa ya Kinondoni Yusufu Mwenda akiwa na watendaji wa soko hilo akizungumza mara baada ya kukagua  vizimba vyo soko hilo kabla ya kuwakabidhi wafanya biashara.
 
2
Baadhi ya wafanyabiashara wakiwa katika zunduzi huyo.
………………………………………………………………….

Na Mwandishi wetu

MSTAHIKI  Meya wa manispaa ya Kinondoni, Yusufu Mwenda  amesema kuwa soko jipya la SIMU 2000 litaweza kuchukua wafanyabiashara 512 kutoka kila pembe ya manispaa ya kinondoni.

Mwenda amewatoa hofu wafanyabiashara wa soko jipya la kituo cha basi cha Simu2000 mawasiliano  kuwa watafanya biashara bila ya kuwa na matatizo yoyote kwa kuwa soko hilo lipo katika mfumo wa kisasa.

Mwenda alisema hayo alipokuwa akikabidhi vizimba vya soko hilo kwa wafanya biashara ndondogo waishio katika wilaya ya kinondoni na sio mtu kutoka eneo la nje ya manispaa hiyo hivyo kuwataka kulitunza soko hilo kama mali yao.

“tumeamua kulifanya soko hili hili liweze kuanza kazi kabla ya uzinduzi rasmi utakaofanywa baadae hili kuweza  kuwapa fursa wafanya biashara kuliko kuacha jingo limeisha na kuonekana kama picha hivyo nawaomba mfanye biashara hili muweze kujiongeza kipato” alisema Mwenda.

Alitoa wito kwa wafanyabiashara hao kutokata tamaa kwani mwanzo ni mgumu kwani eneo lenyewe ni jipya hivyo sio rahisi kuona biashara ikichanganya kwa haraka kama wanavyofikiri.

Mstahiki Meya aliwataka wafanyabiashara hao kuanza biashara mara moja ili kutimiza lengo la kujengwa kwa soko hilo.

Mmoja wa wafanyabiashara ndogondogo aliyepata nafasi katika soko hilo aliishukuru manispaa ya Kinondoni  kwa kuona umuhimu wa kujenga soko hilo, kwani pamoja na kuwaongezea wao vipato kwa kufanya biashara pia itasogeza huduma karibu hata kwa abiria na majirani wa kituo hicho cha Sinza Bus Terminal.

No comments

Powered by Blogger.