Header Ads

WAZIRI BERNARD MEMBE AMETOA RAI KWA WATANZANIA KUTOCHAGUA VIONGOZI WALA RUSHWA



ME1
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akionyesha tuzo maalumu baada ya kupokea kutoka kwa Sheikh Ismail Mohamed wakati wa tamasha la kwanza la Kaswida lililofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa na kudhaminiwa na Kampuni ya Dira ya Mtanzania.

ME2
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akipokea tuzo maalumu kutoka kwa Sheikh Ismail Mohamed wakati wa tamasha la kwanza la Kaswida lililofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa na kudhaminiwa na Kampuni ya Dira ya Mtanzania.

ME3
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akimsikiliza Sheikh Ismail Mohamed akizungumza katika tamasha hilo 

ME8
 Mwimbaji wa Qaswida Rahma Muhidin akiimba Qaswida katika Tamasha hilo

ME9
Mshiriki wa uimbaji wa Qaswida Rahma Muhidin akiimba katika tamasha hilo.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Ulamaa Qaswida Promotions ambao ndio waandaji wa tamasha la kwanza la Qaswida,Ustaadh Jumanne Ligopora akimkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatifa, Mh.Bernard Membe

Na Mwandishi wetu
 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akizungumza katika tamasha hilo la kwanza Qaswida, lililofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Benjamini Mkapa,Mh Membe amewataka Watanzania kusubiri kwa hamu siku ya kutangaza nia ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Alisema siku hiyo ya Juni 6, wananchi wasikilize nini anataka kuifanya nchi iweze kuondoka ilipo ikiwemo kuendelea kudumisha amani na utulivu uliopo. “Mkae tayari siku hiyo, naamini uongozi mzuri wa nchi ni ule wa kudumisha amani na utulivu na ili nchi iweze kusonga mbele, maadili kwa viongozi ni muhimu,” alisema Waziri Membe.

Membe alitumia nafasi hiyo kuwasihi Watanzania kuacha kuchagua viongozi ambao kwa nje, wanajinadi wana dini, lakini matendo hayaendani na maadili ya dini zao. Alisema ili mtu aweze kuaminika kuwa ana dini, jamii ifuatilie katika madhehebu yao, hivyo amewasihi wasichague viongozi wanaosaka uongozi kwa kutoa rushwa.

“Msikubali kuwa na viongozi ambao kwa nje, wanaojinadi kuwa na dini kinyume na matendo yao, lazima mchague wenye hofu ya Mungu ambayo husisitizwa na dini zote,” Alisema uongozi wa heshima ni ule unaochukia rushwa ambayo ni adui wa haki, hivyo amewataka wananchi kuwaogopa wapenda rushwa kama ukoma.




No comments

Powered by Blogger.