Header Ads

MKOA WA DAR ES SALAAM, WAMDHAMINI WAZIRI WA MAMBO YA NJE, BERNARD MEMBE

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akionyesha fomu zilizojazwa na wanaCCM wa Mkoa wa Dar es Salaam zaidi ya 1,500 kwa ajili ya kumdhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kushoto ni mkewe Mama Dorcas Membe. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akizungumza na umati wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliofurika katika ukumbi wa Vijana Kinondoni mkoani Dar es Salaam Juni 25.2015, kwa ajili ya kumdhamini.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akiagana na umati wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliofurika katika ukumbi wa Vijana Kinondoni mkoani Dar es Salaam Juni 25.2015, waliofika ili kumdhamini. 

No comments

Powered by Blogger.