Header Ads

CHANJO YA WATOTO YAZINDULIWA WILAYANI NGARA

1
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizindua rasmi Chanjo ya  watoto kuzuia maambukizi ya magonjwa katika kata ya Nyakisasa kijiji cha Kashinga akiwa katika ziara yake ya kikazi wilayani Ngara mkoani Kagera lengo la ziara hiyo likiwani ni kukagua utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010 na kuhimiza uhai wa chama, Katika ziara hiyo Kinana anaongozana na Nape Nnauye na viongozi mbalimbali wa CCM  kutoka mkoa wa Kagera.

Wanaoshuhudia tukio hili nyuma ni Mh. John Mongela Mkuu wa mkoa wa Kagera na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera Mama Costansia Buhie.

Wakati huo huo Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Ngara amesema Mamlaka ya Mapato TRA na Kikosi cha Usalama barabarani wana kila sababu ya kupeleka huduma zao utoaji wa leseni za udereva na huduma za usajiri wa vyombo vya moto mikoani na wilayani kwani ni usumbufu mkubwa wanaopata wananchi kufuata huduma hizo za Leseni za kuendesha vyombo vya moto na usajiri wa vyombo hivyo.

Amezitaka taasisi hizo kufanya hivyo ili kuwaondolea wananchi usumbufu wanaoupata wanapohitaji huduma hizo kutokana na umbali, Wananchi wa Ngara wanalazimika kufuata  huduma hiyo Bukoba mjini jambo ambalo linawaletea wananchi hao usumbufu mkubwa na upotevu wa fedha bila sababu ya msingi.
 
2
Baadhi ya akina mama na watoto wao wakisubiri watoto wao kupatiwa chanjo katika zahanati ya kijiji chaKashinga wilayani Ngara.

3
Mh. John Mongela Mkuu wa mkoa wa Kagera akiungumza jambo huku Nape Nnauye akimsikiliza.

4
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera Mama Costansia Buhie wakati alipokuwa akimkaribisha ili kuzungumza na wananchi katika zahanati ya Kashinga.

5
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi hawapo pichani wakati alipozindua chanjo ya watoto katika zahanati ya Kashinga akiwa katika ziara ya kikazi wilayani Ngara leo wa tatu kutoka kulia ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM na katikati ni  Mkuu wa mkoa wa Kagera Mh. John Mongella

6
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda mti wa kumbukumbu katika zahanati hiyo. 

7
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na viongozi wa CCM wilayani Ngara wakishiriki kwa pamoja katika ujenzi wa ofisi ya CCM tawi la Munjebwe Rulenge.

8
Nape Nnauye akiwahutubia wananchi katika soko la Rulenge leo wakati Kinana alipofanya ziara ya kikazi katika kata hiyo.

9
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Rulenge.

10 11
Umati wa wananchi waliohudhuria katika mkutano huo.

12
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi mbalimbali za waliokuwa wanachama wa Chama cha CHADEMA mara baada ya kurejesha kwake na kujiunga na CCM katika mji wa Rulenge.

13
Baadhi ya kadi zilizorejeshwa kwa Kinana na wananchi hao na kujiunga na CCM.

14
Kwaya ya akina mama wa Rulenge wakiimba wimbo maalum wakati wa mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati wa mkutano wa hadhara.

15
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza  mzee Dodwin Magambo wakati alipowasilisha malalamiko yake kwake.

16
Mtambo wa umeme  vijijini REA unaojengwa katika kijiji cha Djuruligwa kata ya Kabanga.

17
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua Mtambo wa umeme  vijijini REA unaojengwa katika kijiji cha Djuruligwa kata ya Kabanga

18
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na mhandisi wa kampuni ya kichina ya TKPE Bw.Ton Minyang wakati alipokagua ujenzi wa  Mtambo wa umeme  vijijini REA unaojengwa katika kijiji cha Djuruligwa kata ya Kabanga

19
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizindua kkikundi cha akina mama wajasiriamali cha mjini Ngara kabla ya kuhutubia mkutano wake na wananchi mjini humo leo.

20
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata keki kuashiria uzinduzi wa kikundi hicho cha akina mama wajasiriamali.

21
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi wakati alipokuwa akiwasili katika mkutano wa hadhara mjini Ngara leo.

22
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinan akiangalia vikundi vya ngoma mara baada ya kuwasili katika mkutano huo. 

23
MNEC wa wilaya ya Ngara Bw. Issa Samma akizungumza na wananchi wa mjini Ngara wakati wa mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.

24
Nape Nnauye akimwaga sumu kwa wana Ngara na kuwaambia waitunze amani waliyonayo kwani wao wanajua machungu ya amani kuvurugika katika nchi kutokana na uzoefu wao wa kupokea wakimbizi kutoka nchi mbalimbali jirani.

25
Nape Nnauye akisisitiza jambo wakati alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara mjini Ngara.

26
Umati wa wananchi ukisikiliza hotuba za viongozi mbalimbali waliohutubia katika mkutano huo.

27
Mkuu wa wilaya ya Ngara akizungumza jambo na wananchi

28
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinan akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Ngara leo

No comments

Powered by Blogger.