Header Ads

KATIBU MKUU WA CCM, ABDULRAHMAN KINANA AWASILI WILAYANI MISUNGWI MKOANI MWANZA

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Diwani ya Kata ya Kalebezo ,Sengerema Ndugu Joseph Yaledi muda mfupi kabla ya kupanda kivuko kuelekea wilaya ya Misungwi.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (aliyeweka mikono mifukoni) akipanda kivuko cha Misungwi kuelekea wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye kivuko cha Misungwi pamoja Mbunge wa Sengerema Wiliam Ngeleja (kushoto) na Diwani wa Kalebezo Ndugu Joseph Yaledi na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Sengerema Ndugu Chasama Kamata, wengine wanaonekana nyuma yao ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ,na Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza Ndugu Miraji Mtaturu (kulia).

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiteremka kutoka kwenye kivuko cha MV.Misungwi.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Misungwi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Mhe. Charles Kitwanga wakati wa mapokezi Usagara wilaya Misungwi.

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Misungwi Bernard Polycarp wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM katika kata ya Usagara wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.

 Katibu Mkuu wa CCM akiangalia vikundi vya utamaduni wakati wa mapokezi.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi waliojitokeza kumpokea kwenye kata ya Usagara.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuweka dirisha katika zahanati ya Nyang'homango wilaya ya Misungwi mkoa wa Mwanza.

 Ofisi ya CCM Tawi la Nyang'homango

 Mbunge wa Jimbo la Misungwi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Mhe. Charles Kitwanga akisalimia wananchi wa kijiji cha Nyang'homango nje ya jengo la ofisi ya Tawi la CCM.

Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana akiweka jiwe la ufunguzi wa ofisi ya Tawi la CCM Nyang'homango wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimkabidhi kadi ya uanachama wa CCM Bi.Agness Nestrory wa kijiji cha Nyang'homango ambapo zaidi ya wanachama 400 walijiunga na CCM.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wakazi wa kijiji cha Nyang'homango wilaya ya Misungwi mara baada ya kufungua ofisi ya CCM tawi.

(Picha zote na Adam Mzee)

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

No comments

Powered by Blogger.