Header Ads

WANANCHI WA WILAYA YA NYAG'HWALE MKOANI GEITA, WAFURIKA KUMSIKILIZA KATIBU MKUU WA CCM, KOMREDI KINANA

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Nyang'hwale Mhe.Hussein Nassoro Amali wakati wa mapokezi katika kata ya Bukwimba wilaya ya Nyang'hwale mkoani Geita.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishukuru kwa mapokezi mazuri kata ya Bukwimba.


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wakazi wa kata ya Bukwimba ikiwa sehemu ya ziara yake ya kujenga na kuimarisha Chama mkoani Geita.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipaka rangi ukuta rangi jengo la ofisi ya chama kata ya Bukwimba,jengo hili lilijengwa mwaka 1966 na linatumika mpaka sasa.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Nyang'hwale Mhe.Hussein Nassoro Amali(katikati) pamoja na Diwani kata ya Bukwimba na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale Mhe.Yavin Noah.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Nyakwasi wilaya ya Nyang'hwale mkoani Geita.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiswaga Ng'ombe kuingia kwenye josho katika kijiji cha Nyakwasi, Nyng'hwale mkoani Geita.

 Mbunge wa Jimbo la Nyang'hwale Mhe.Hussein Nassoro Amali akizungumza na Nyamgogwa kabla ya kuzindua mradi mashine za kukoboa mpunga na kusaga mahindi wa akina mama cha UWT ambacho kina wanachama 100.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinanaakiangalia baadhi ya miradi ya akina mama wajasiriamali wa Nyang'hwale.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimu wakazi wa kata ya Nyijundu.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Nyijundu, wilaya ya Nywang'hwale mkoani Geita ambao kwa ushirikiano wa wananchi na Mbunge wao wameweza kujenga madarasa mengi ya shule ya sekondari ya kata ya Nyijundu.

Wananchi wa Kata ya Nyijundu wakinyoosha mikono juu kama ishara ya kukubali kazi inayofanywa na Chama cha Mapinduzi.

Diwani wa Kata ya Nyijundu Jacob Daniel Nyanda akizungumza na wakazi wa kata yake na kutoa shukrani kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwa kutembelea na kujionea ujenzi wa shule ya sekondari.Nyijundu, wilaya ya Nyang'hwale ,Geita.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (katikati) akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Nyang'hwale Mhe.Hussein Nassoro Amali (kushoto) na M-NEC wa Nyang'hwale Mhe. James Musalika.

 Kaimu Mkuu wa mkoa wa Geita ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Nyang'hwale akihutubia wananchi wa kaa ya Kharumwa waliojitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa michezo wa Kharumwa ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.

 Wananchi wa Kharumwa wakimsikiliza Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
 Katibu wa Itikadi na Unezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Kharumwa na kuwaambia kuwa Kiongozi ni mtu mwenye moyo wa uvumilivu na usikivu, kiongozi wa siasa hapaswi kuwa na mashitaka ya kupiga watu.

 Wananchi wa kata ya Kharumwa wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Kharuma ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa ili nchi isonge mbele inabidi matumizi yasiyo ya lazima yapunguzwe na vijana kuami kuwa maisha ni kuchapa kazi na si kukaa vijiweni,aliwataka wananchi hao kuchagua viongozi wenye moyo na watu.

Mbunge wa Jimbo la Nyang'hwale Mhe.Hussein Nassoro Amaliakihutubia wakazi wa Kharumwa kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliokusanya wananchi wengi kuliko kawaida.

Mbunge wa Jimbo la Nyang'hwale Mhe.Hussein Nassoro Amali akiwatangazia wananchi wa kata ya kharumwa kuwa atagombea tena Ubunge wa jimbo hilo.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

No comments

Powered by Blogger.