Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA atembelea Kiwanda cha Sukari Cha Alteo, MAURITIUS
..............................
Waziri Kassim Majaliwa ametembelea kiwanda cha sukari cha Kampuni ya Alteo ya Nchini
Mauritius chenye uwezo wa kukamua tani 400 za miwa kwa saa na kuzalisha tani
170,000 za sukari kwa mwaka.
Kampuni
ya
Alteo inamiliki kiwanda cha sukari cha TPC mkoani Kilimanjaro kwa ubia
na Serikali ya Tanzania na kinazalisha tani 110,000 kwa mwaka.
Waziri Mkuu ametembelea
kiwanda hicho leo (Jumanne, Machi 21, 2017) na kujionea namna wanavyozalisha
sukari kwa kutumia teknolojia ya kisasa.
Aidha, Waziri
Mkuu amefanya mazungumzo na uongozi wa kiwanda hicho na kuwashawishi waongeze
maeneo ya uwekezaji nchini.
“Tekonolojia
wanayoitumia katika uendeshaji wa kiwanda chao ni nzuri hivyo tumewashawishi
waje kuongeza maeneo ya uzalishaji wa sukari nchini ili tuweze kukidhi
mahitaji,” amesema.
Waziri Mkuu
amesema Tanzania kuna viwanda vitano vya sukari ambavyo ni Mtibwa, Mahonda
(Zanzibar), TPC, Kilombero na Kagera
vinavyozalisha tani 320,000 kwa mwaka huku mahitaji ni tani 420,000.
Kwa upande
wake Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Khalid Salum Mohammed amesema Zanzibar
kuna kiwanda kimoja cha sukari ambacho uzalishaji wake haukidhi mahitaji
kutokana na
uhaba wa
malighafi.
Kutokana na
hali hiyo, Dkt. Khalid ameikaribisha kampuni ya Alteo kwenda Zanzibar
kushirikiana na Serikali katika uwekezaji hususani kwenye viwanda vya
sukari.
Naye Mtendaji
Mkuu wa Kampuni hiyo Bw. Patrick de Labauve amesema wamekubali kuongeza maeneo
ya uwekezani wa mashamba ya miwa nchini.
Pia ameomba
Serikali iwapatie fursa ya uwekezaji katika sekta ya utalii mkoani Kilimanjaro.
“ Kuna vivutio vingi vya utalii ukiwemo mlima Kilimanjaro,”.
Akizungumzia
kuhusu ajira amesema kiwanda cha TPC kimeajiri wafanyakazi 3,000 wakiwemo 1,900
wa kudumu.
Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akikagua shamba la miwa wakati alipotembelea kiwanda cha sukari cha Alteo nchini Mauritius Machi 21, 2017. |
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea kiwanda cha sukari cha Alteo nchini Mauritius Machi 21, 2017. |
Post a Comment