Header Ads

Naibu Waziri SELEMANI JAFO akagua Maendeleo ya Ujenzi wa Daraja la Toangoma

 Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Suleiman Jaffo (katikati) akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Mbagala, Issa Mangungu alipokwenda kukagua ujenzi wa daraja linalounganisha Kata za Toangoma na Kijichi, Dar es Salaam leo, Kushoto ni Diwani wa Kata ya Toangoma, Mohamed Mketo. 

Na Dalila Sharif

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo amekagua ujenzi wa Daraja linalounganisha Kijichi hadi Toangoma wilayani Temeke.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam leo, alipokuwa akikagua ujenzi wa daraja hilo, Naibu Waziri alisema ameridhishwa na maandalizi ya ujenzi wa daraja hilo

“Daraja hilo lenye urefu wa mita 600 na inatakiwa matayarisho yaanze mapema kwa kuchonga barabara  ili ujenzi ukamilike mapema tayari kwa wananchi kulitumia,”alisema Jafo.

Mkuu wa Wilaya  hiyo, Felix Lyaniva alisema anampongeza Naibu Waziri kwa kukagua ujenzi wa daraja hilo kwa kuwa ni nia njema katika kuendeleza maendeleo ya wilaya hiyo.

“Wapo katika harakati za mandalizi ya ujenzi wa daraja hilo litakaloweza kusaidia kupunguza kero za wananchi wanaotembea umbali mrefu kwa miguu katika maeneo hayo,”alisema Lyaniva.

Hata hivyo, Mbunge wa Jimbo la Mbagala, Issa Mangungu alimuomba waziri  kuwatatulia wananchi wa eneo hilo  kero inayowakabili ya kutolipwa fidia zao.


“Wakazi wa eneo ambao hadi sasa hawajalipwa fidia ya nyumba zao wamekuwa wakikumbwa na mafuriko yanayosababishwa na mvua hivyo kuathirika kwa kiasi kikubwa,”alisema Mangungu.


 Mbunge wa Jimbo la Mbagala, Issa Mangungu akifafanua jambo kwa wanahabari kuhusu maendeleo ya mradi huo.


 Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Suleiman Jaffo akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Mbagala, Issa Mangungu alipokwenda kukagua ujenzi wa daraja linalounganisha Kata za Toangoma na Kijichi, Dar es Salaam leo. Kushoto ni Diwani wa Kata ya Toangoma, Mohamed Mketo. 

Jaffo akitoa maagizo baada ya kukagua mradi huo.

No comments

Powered by Blogger.