Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Josephine
Matiro katika Uwanja wa Ndege wa Mgodi wa Buzwagi 27March2017 katikati ni Mkuu wa Mkoa
wa Shinyanga Zainabu Telaki Viongozi hao walifika kumpokea Waziri
Mkuu alipofika kuangalia shughuli za Mgodi wa Buzwagi uliopo wilaya Kahama Mkoa
wa Shinyanga. .....................................................
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amefanya ziara kwenye mgodi wa dhahabu wa Buzwagi
uliopo wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga na kuchukua sampuli za mchanga
katika makontena mbalimbali kwa lengo la kwenda kuyapima kwa wataalamu
wa madini ili kubaini kiasi cha dhahabu kilichomo.
Amesema
wanataka kuona mchanga unaosafirishwa na mwekezaji huyo unakiasi gani
cha dhahabu, pia Serikali inataka kufahamu kama kodi inayolipwa ni
sahihi.” Hata hivyo tayari Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli alishatoa
tangazo la kuzuia usafirishaji wa michanga kwenda nje ya nchi,”.
Waziri
Mkuu alitembelea mgodi huo jana jioni (Jumatatu, Machi 27, 2017) na
kuchukua sampuli za mchanga kwa lengo la kuondoa mashaka juu ya
kinachosafirishwa. Sampuli hizo amezichukuwa kwenye makontena
yaliyofungwa kwa ajili ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi.
“Tumeamua
kuchukua sampuli za mchanga ambao mwekezaj anasema wanaupeleka nje ya
nchi kwa ajili ya kwenda kutenganisha madini ya dhahabu na shaba. Hata
hivyo nimemuhoji kwa nini mitambo hiyo isiletwe nchini ili kila kitu
kifanyike hapahapa,”
Waziri
Mkuu amesema sera ya uwekezaji inasema mtambo huo unatakiwa uwepo
nchini ili kila hatua ya uchenjuaji ifanyike hapa hapa, hivyo tunataka
kujiridhisha na mwenendo wa mwekezaji na mapato tunayoyapata kama
yanastahili.
|
Post a Comment