Header Ads

Mashirika ya Umma yatakiwa Kujiandaa Kuchangia Bajeti ya Serikali

 mkurugenzi miliki na miradi wa miradi wa kituo cha mikutano cha AICC Victoria Kamagenge akiwa anawaonyesha kamati Ya uwekezaji wa mitaji ya uma  PAC moja ya mradi unaojegwa na kituo cha mikutano cha AICC  jijini Arusha mradi unaogarimu kiasi cha shilingi bilioni 2.8.
...........................

Na Woinde Shizza,Arusha

Kamati ya Bunge ya Uwekezaji Mitaji ya Umma (PAC) imeyataka mashirika ya umma 265 yalilopo hapa nchini, kuanza kujiandaa kuchangia bajeti ya  serikali kuanzia mwaka ujao wa fedha .

Aidha wakurugenzi na wenyeviti wa bodi wa mashirika hayo kuanzia mwakani  watatakiwa  kuwasilisha bajeti zao bungeni ili kuweza kupitishwa na bunge na hakuna shirika lolote la serikali litakaloweza kupiitishwa  bajeti bila kuithinishwa  na bunge.

Hayo yamebainishwa na mwenyekiti  wa kamati hiyo  ,Albart Obama Mtabaliba mbunge wa jimbo la Buhigwe, mkoani Kigoma, wakati kamati hiyo ilipotembelea miradi ya kituo cha kimataifa cha mikutano (AICC)nakujionea miradi mbalimbali inayoendeshwa na kituo hicho ikiwemo ujenzi wa nyumba za kupangisha ,hospitali pamoja na jengo la maonyesho na mikutano linaloendelea kujengwa na kituo hicho.

Alisema kuwa  licha ya mashirika hayo kuwa na thamani kubwa ya shilingi trilioni 26 lakini yamekuwa hayachangii ipasavyo bajeti ya serikali ,hivyo yanatakiwa  yabadilike na kuanza kulipa kodi ipasavyo pamoja na kutoa gawio serikalini.

‘’Mashirika yote ya umma yaliyopo hapa nchini yanadhamani ya shilingi trilioni 26 na kwa mwaka yamekuwa yakitoa faida ya shilingi bilioni 450 pekee ,ambayo ni sawa na asilimia 1.08% kitu ambacho hakiwezekani ukilinganisha na mtaji uliopo wa trilioni 26  ,na hivyo wakurugenzi na wenyeviti wa bodi wametakiwa wahakikishe mapato yao kwa serikali yanapanda na angalau weweze kuchangia trilioni mbili kwa mwaka “alisema Mtabaliba.

Akizunguzia kituo  cha mikutano cha kimataifa  AICC alipongeza miradi inayoendeshwa na kituo hicho na kushauri  waanze kuchukuwa hatua ya kuanza kukabiliana na soko na pia wajitahidi kuwekeza zaidi katika ujenzi wa vituo vya mikutano vya kisasa ,na kuwataka kuelekeza nguvu zaidi ya kujenga kituo kikubwa cha mikutano katika mji mkuu wa Tanzania  ambapo ni Dodoma.

Hata hivyo mmoja wa  wabunge wa  kamati hiyo,Ester Bulaya alikosoa  gharama za ukarabati zilizotumika kukarabati ukumbi wa Simba hall  uliopo katika kituo hicho ambapo kiasi cha shilingi bilioni tatu na nusu zilitumika jambo ambalo hawakuafiki na kushauri kwamba fedha hizo ninyingi sana na zingeweza kutumika kwenye uwekezaji mwingine .

Naye mkurugenzi mtendaji  wa AICC  Elishilia Kaaya  alisema kuwa amefurahishwa  na ujio wa kamati hiyo kuwatembelea  na pia wamekutana nao na wamepewa elimu nzuri ya uwekezaji na wametaza baadhi ya  mambo yale ambayo ayajaenda sawa wamewarekebisha pale ambapo awapo vyema wamewafundisha hivyo wanaamini  walivyoambiwa mtazamo ubadili utabadilika kulingana na hali ilivyo.

Hata hivyo alisema kwa sasa wameanzisha mradi ujenzi wa kumbi za mikutano,mahoteli na maonyesho  unaogarimu kiasi cha shilingi shilingi bilioni 2.8,mradi ambao unatarajiwa kukamilika mapema May 4 ambapo wanategemea utasaidia kuongeza mapato ya kituo hicho pamoja na ajira kwa watanzania.


 Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji Mitaji ya Umma (PAC) wakiwa wanateta jambo.


 Wakiendelea kukagua.

 Mbunge wa jimbo la Bunda mjini  Ester Bulaya akiwa anakula na wakandarasi wa jengo jipya la maonyesho linalojengwa na kituo cha mikutano cha AICC wakati walipofanya ziara na Kamati ya Bunge ya Uwekezaji Mitaji ya Umma ( PAC ).


Kamati ya Bunge ya Uwekezaji Mitaji ya Umma (PAC) wakiwa katika picha ya pamoja.

No comments

Powered by Blogger.