Soko la Mbao ladaiwa Kushuka Wilayani Mufindi
Mbunge wa
mafinga mjini Cosato Chumi akiongea na Wafanyabiashara wa mazao ya
misitu wilayani Mufindi juu ya malamiko yao kwa TRA mkoa wa Iringa.
Baadhi ya wafanyabiashara wa mazao ya
misitu wilayani Mufindi waliohudhulia mkutano wa pamoja kati ya mbunge,TRA na wafanyabiashara.
...................................
Na Fredy Mgunda,Mufindi
Wafanyabiashara wa mazao ya
misitu wilayani Mufindi wamesema kuwa soko la mbao limeshuka kwa kiwango
kikubwa kutoka na mrundikano wa kodi katika wilaya hiyo tofauti na wilaya
nyingime.
“Ukienda mbeya,njombe na
maeneo mengine kodi ya vibali ni ndogo kuliko ya hapa mufindi sasa tunataka
kujua tatizo nini”walisema wafanyabiashara
Aidha wafanyabiasha hao wameiomba
mamlaka ya mapato mkoa wa iringa TRA kutoa kibali cha usafirishaji kwa kuondoa usumbufu wa tozo za ushuru check
point na kuombwa lisiti za mashine kutoka kwa wakulima waliowauzia mbao na
nguzo.
Akizungumza mmoja wa
wafanyabiashara hao Zakayo Kenyatta Katika mkutano wa wafanyabiashara wa mazao
ya misitu na TRA alisema kuwa TRA wamekuwa wasumbufu sana check point kwa
kuwasimamisha zaidi ya siku tatu wakidai lisiti hizo huku wafanyabiashara
wakionyesha barua za watendaji kutoka vijiji walivyonunulia zikikataliwa.
"Tunawaomba TRA mkatoe
elimu kwa mkulima mmoja mmoja kwa sababu ni ngumu sana mkulima wa chini akuulizie nguzo 5 alafu awe na lisiti
ya mashine kwa hiyo tunawaomba TRA wakatoe elimu hiyo na kuwaamasisha wakulima
hawa Kuwa na hizo mashine kwani wakulima hao ni wale ambao wanauza miti yako
kutokana na matatizo mbali mbali walionayo na sio kampuni" alisema
Kenyatta.
Akijibu hoja hiyo meneja
msaidizi wa TRA iringa Mustapha Mkilamwenye alisema Kuwa wamekuwa
wakiogopa kwenda kutoa elimu hizo kwa wakulima kutokana na mkutano yao
kuharibika kwa kuzomewa na kutokufikia muafaka WA uelimishaji.
Pia Mkilamwenye amewataka
wafanyabiashara hao kupata kibari cha kununua na kusafirisha kutoka TRA wilaya
au mkoa kabla hqwqjaenda vijijini kununua ili kukwepa uwumbufu huo check point.
"Ombi lenu tumelipokea
hivyo tunawaomba kabla hamjanunua mpate kibali kutoka TRA mkoa au wilayani
kuokoa usumbufu WA tozo za ushuru check point, pia tutatoa elimu ya matumizi ya
mashine kwa wakulima vijijini wauzapo miti yako kwa wafanyabiashara"
alisema
Post a Comment